ad

ad

Kumbe Vikiungwa Vitamu - 04






 ILIPOISHIA
“Mbona hivyo mama yangu”
“Kazi gani ya kutoka saa moja asubuhi kurudi saa tano za usiku?”
Mmh, makubwa nimekuwa mtoto mdogo wa kuwa chini yake kwa kila kitu. Nilijua uchawi wa Bi Shuu ni nini, niliinama na kuchukua mkoba wangu na kufungua. Nilihesa nyekundu tano na kumpa.
“Za nini?”
“Katumie tu”
“Za kodi?”
“Walaa, nimekutunuku tu mama yangu.”
“Kweli!?”
“Kweli unafili uliyonifikiza madogo”
Bi Shuu alifurahi na kunikumbatia na kusahau aliyobwatuka muda mfupi, baada ya kunipandisha na kunishusha alisema.
“Weee mwana kulikoni”
“Kaa chini nikupashe kazi imekuwa kaziiiii”
“Usiniambie”

“Habari ndiyo hiyo shilingi moja kwa sekunde ndio mpango”

“Wacha wee leo Mchaka kawa mzaramu”

“Umenifundisha wewe, ngoja nikaoge nikupashe upashike”

Nilimuacha Bi Shuu chumbani kwangu akizirudia kuzihesabu pesa nilizompa mimi nikaenda kujimwagia maji.

Nilipotoka kuoga nilimkuta akinisubiri kwa hamu kubwa.

“mmhu, hebu nipe raha”

“Bi shuu nitakueleza yote kesho”

“Mwana wee siwezi kulala mpaka unipe siri ya rangi nyekundi kupendeza na kusikitisha”

Huku nikijifuta maji nilimueleza yote bila kumficha hata moja, mwisho wa yote nilielezea masikitiko yangu ya bahati ya kupendwa na mkosi wa kuachwa.

“Bi Shuu, japo nimepata lakini wasiwasi wangu sichelewi kumwagwa”

“Kwani una tatizo gani?”

“hata silijui hakuna hata mwanaume mmoja aliyenieleza tatizo langu”

“Mmh, kuna umuhimu wa kulifanyia kazi”

“Siamini kama tatizo langu litaisha”

“Hebu kila ukiwa na huyu bwana msikilie na muulize an apenda nini chochote usimnyime”

“mmh, Bi Shuu wanaume wengine waharibifu ukimchekea anakuharibu”

“Sio unavyo fikiria’

“Kuna nini wanaume wanacho taka zaidi ya kuwaharibu wanawake, sijazaa babu wee cha kuwekewa matambala”

“Sina maana hiyo si wote wana penda mchezo huo.”

“mmh, nitamsikiliza”

“Sasa mwana wee lala nakuomba muheshimu mpenzio kama Mungu wako huoni muda si mrefu nasi tutatembelea gari”

“Ndicho ninachokiomba, sijui yatakuwa yale yale.”

“Basi mwali lala usingizi unono.”

“Nawe pia Bi shuu”

Bi Shuu aliniaga na kuondoka na kuniacha nikimalizia kujifuta maji ili nilale.

                                                            ******

Siku ya pili wakati namalizia kujipodoa kabla ya kwenda kujifusha udi kwa Bi Shuu simu ya Mateja iliingia, niliipokea na kuzungumza naye.

“Haloo ma’ Sweet.”

“Ooh, ma honey girl.”

“Ni mimi, mhu baba nipe habari naona simu za asubuhi asubuhi?”

“Aah, kawaida ila kuna dereva nimemtuma atakupitia muda si mrefu.”

“Hakuna tatizo Sweet.”

Baada ya Mateja kukata simu, kwa vile nilikuwa tayari nimeisha jipodoa nilikwenda chumbani kwa Bi Shuu. Kabla ya kuingia nilikutana na moto uliokuwa ukinukia vizuri, harufu ya asubuhi ile ilikuwa zaidi na ya jana yake

Niliingia na kumkuta akiweka udi kwenye kitezo, aliponiona alitabasamu na kusema.

“Haya mwali jifushe uwahi kazini.”

Niliinama na kufunikwa shuka ili moshi wote wa harufu nzuri uishie kwenye nguo na mwilini, baada ya muda alifunua shuka na kuninusa kama mbwa anayesaka chakula jaani. Asikuambie mtu Bi Shuu havumi lakini yumo, mtu mzima lakini ovyooo.

“Umevaa kufuri gani?” Bi Shuu aliniuliza swali ambalo sikufikiria kuniuliza.

“Nyeupe.”

“Hebu nione.”

Mmh, makubwa nilinyanyua gauni na kuiona nilikuwa nimevaa kufuli la mikanda ‘Bikini’.

“Mwali ndio nini?” Bi Shuu alishtuka.

“Mbona umeshangaa?”

“Unakwenda kwenye starehe au kazini?”

“Kazini.”

“Sasa mbona umevaa kufuri kama unakwenda kwenye kilimo cha mihogo.”

“Babu weee kwenda na wakati.”

“Acha ushamba vaa kufuri la kawaida, hilo kufuri unalivaa siku unayokutana na mpenzi ukitoa nguo tu akiona anaingia kimuhemuhe.”

Mmh, sikutaka kubishana naye nilirudi hadi chumbani kubadili kufuri, wakati namaliza kuvaa honi ya gari ilipigwa nje nilijua  mtu aliyetumwa kunifuata amefika. Nilikimbilia chumbani kwa Bi Shuu kumuaga.

“Bi Shuu naondoka.”

“Umebadili kufuri?”

“Ndiyo.”

“Hebu nione.”

Nilinyanyua tena gauni na kunitazama, nilikuwa nimevaa ya kawaida tena ya rangi nyekundu, alipoiona alisema.

“Ewaaa, sasa hapo ndipo nilipopataka.”

“Basi nawahi kuna mtu ananisubiri hapo nje katumwa na mzee,” nilisema huku nikiteremsha gauni ili niwahi nje.

“Wee Manka ndio nini?”

“Vipi tena Bi Shuu mwenzio nachelewa kazini.”

“Hebu jifushe na hiyo kufuri linukie.”

Nilirudi haraka na kuchutama kwenye kitezo kwa kulitanua gauni langu moshi wote uingie chini. Baada ya kufanya yote niliyoelekezwa na Bi Shuu nilimuaga kwa kumbusu kisha nilipitia mkoba wangu na kutoka nje. Nilimkuta gari likinisubiri, niliingia kwenye gari na gari liliondoka.

“Mambo?”

“Poa, sijui yako?”

“Hata mimi ipo poa.”

Safari iliendelea hadi ofisini, nilipofika nilipita moja kwa moja hadi ofisini kwa Mateja, alivyokuwa ameisha ingia ofisini. Baada ya kufungua mlango wa ofisi niliingia huku nikiachia tabasamu pana na kutanua mikono yangu, Mateja aliponiona alizunguka meza yake kunipokea. Tulikutana katikati na kukumbatiana.

Tuliporomosheana mabusu moto moto huku tukigandisha midomo kwa muda na kubadilisha mate.

“Mmh, tosha,” nilisema huku nikijitoa mikononi kwa Mateja.

“Mhu, za nyumbani?”

“Mmh, mzuri sijui kwako?”

“Kwangu ilikuwa ngumu kidogo kutokana na kuwa na wakati mgumu baada ya kukuota tupo pamoja niliposhutuka nilijikuta nipo peke yangu.”

“Pole sana, basi ndio ufanye haraka kunichukua.”

“Kwa mateso ya jana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.”

“Basi mengine baada ya kazi.”

“Haya mama, mimi niseme nini.”

Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi.

Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi. Pamoja na furaha ile bado wasiwasi wangu ulikuwa nini hatima yangu kwake, nitaendelea naye au ndiyo atanitosa kama waliotangulia.

ILIPOISHIA

Wazo la awali lilikuwa kuomba msaada kwa Bi Shuu ili niweze kumdhiniti. Niliendelea na kazi zangu kama kawaida, muda wa mchana tulikwenda kula pamoja kama wapenzi wasiojificha.

  Siku ile baada ya kurudi nyumbani aliniomba tuwe wote usiku wa siku ile, sikumkatalia kwa vile ndiye aliyekuwa mmiliki wa mwili wangu. Usiku alinipitia  na kuondoka kwenda kulala naye mpaka asubuhi, kaonja kaona tamu sasa anataka kula kabisa. SASA ENDELEA.....

Ni kweli nilifurahi kulala na Mateja mpaka asubuhi kuonesha jinsi gani alivyopagawa kwangu, lakini usiku kwangu ulikuwa wa karaha sana yaani mambo nisiyoyapenda ya kusumbuana wakati wa mapenzi yalijirudia tena. Nilishindwa kumkatalia kwa vile alikuwa bosi wangu  kwa kuogopa kufukuzwa kazi na maisha ya kutangatanga yalinichosha. Usiku mzima kugeuzwa kama chapati ooh geuka hivi, lala hivi fanya hivyo, basi kero mtindo mmoja. Nilijiuliza bila kunisumbua vile hawezi kukidhi haja zake, mpaka kunakucha nilikuwa nimekasirika mtoto wa kike kila kona ya mwili iliniuma hayakuwa mazoezi bali adhabu ya mapenzi.

Asubuhi Mateja alifurahi sana na kuniahidi kabla ya yote kukibadili chumba changu kwa kuninunulia sofa za nguvu, alinipa pesa nyingi za kutumia na kunirudisha nyumbani. Huwezi amini nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu akinisubiri, kutokana na uchovu nilimsalimia na kuingia ndani nijilaze.

Kabla sijabadili nguo na kuvaa kanga nyepesi Bi Shuu aliingia.

“Mankaaaaa,” aliniita kimbea.

“Unasemaje Bi Shuu,” nilimuuliza huku nikimuangalia jicho zito la usingizi.

“Mmh, sikuwezi.”

“Kwa nini Bi Shuu?”

“Mambo yako mazito.”

“Mmh kawaida tu, vipi ushakunywa chai?”

“Nilikuwa nakusubiri wewe.”

“Mimi kwa sasa hivi siwezi nimechoka sana.”

“Eeeeh Manka weee, mlikuwa mnakomoana.”

“Wee Acha tu,” niliona kama ananichelewesha kulala kutokana na umbea wake wa utu mzima. Nilivuta pochi na kutoa noti kadhaa za kumi kumi na kumpatia Bi Shuu bila kuzihesabu.

“Za nini?”

“Za kwako.”

Bi Shuu alichanganyikiwa na kunivamia kwa furaha na kujitahidi kunibeba japo uzito wangu ulikuwa mkubwa. Kweli pesa sabuni ya roho Bi Shuu alipagawa na kuniona kama malaika niliyetumwa kuja kumpa furaha ya asubuhi ile.

“Bi Shuu niache nipumzike.”

“Mwali weee lala, tena utakutana nimekuandalia chakula kizuuuri.” 

Bi Shuu alitoka na kuniacha nikimalizia kuondoa nguo mwili kisha kuchukua kanga nyepesi kisha kujitupa kitandani. Nililala kwa muda wa saa zaidi ya nane kutokana na uchovu wa mbilinge za Mateja usiku kucha.

Majira ya jioni Mateja alifanya kweli kwa kuleta sofa za nguvu kitu kilichofanya Bi Shuu kunipa chumba kikubwa cha nyumba kubwa. Niliamini ule ulikuwa mwaka wangu wa mimi kurudi katika maisha ya kutanua. Niliamini muda si mfupi lazima niwe na gari langu mwenyewe.

Baada ya kukipamba chumba changu na kupendeza Bi Shuu aliniweka chini na kunipa somo.

“Manka Mungu akupe nini, ukishikwa shikamana mwali wee.”

“Hata mimi najua Bi Shuu.”

“Unaonekana mwanzo ulikuwa ukifanya makusudi mbona sasa hivi mwanaume kapagawa muda si mrefu  utakuwa dunia ya wenye nazo.”

“Ndio maana yake.”

“Basi Manka nitakuongezea vikorombwezo akigusa amenata.”

“Usiniambie!”

“Kwanini wazee wenzangu pamoja na umri wangu wakionja wanapagawa itakuwa wewe ukioga maji yanatelemka.”

“Tena kweli ufanye haraka maana ameisha tangaza ndoa.”

“Basi hiyo kazi niachie.”

Mateja alinipigia simu kuwa siku ile angekuja kulala ili jumatatu twende kazini pamoja nami sikumkatalia. Kweli usiku alikuja kulala kwenye chumba changu kilichokuwa na hadhi kubwa kwa mtu yoyote.  Kama kawaida ya usiku wa jana yake yalijirudi ya kusumbuliwa lala hivi geuka hivi fanya hivi, basi taabu mtindo mmoja.

Na siku ile nilivumilia lakini moyoni nilijisemea siku nyingine nitampasha kweli wake hawezi kunigeuza kama mwanasesele na kunichezea apendavyo.  Nikajikuta siyachukia mapenzi na kuyaona kwangu ni karaha na si starehe, mwanaume alikuwa akipanda juu ya mnazi hashuki mpaka nahisi kichefuchefu.

Niliamini kabisa alitaka kunikomoa kwa vitu alivyonipa, kwangu sikuona mapenzi zaidi ya mateso. Uvumilivu uliponishinda nilianza kuwa mkali kwa kumgomea kwa usumbufu wake kwa kumueleza makavu kuwa sitaki kama hawezi kifo cha mende tuache.

Mateja alinielewa na kustarehe bila usumbufu, nilishangaa kumbe anaweza kukwea mnazi bila kujifunga kamba za miguu. Kilichonishangaza ndani ya mapenzi yetu yaliyochukua miezi minne,  Baadhi ya mambo yalianza kutoonesha dalili zozote za kutimiza ahadi yake.

Siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo uhusiano na Mateja ulivyozidi kulega, hata kuwa pamoja baada ya kazi ikafutika kila muda alionekana yupo bize. Kitendo cha kutokuwa karibu na Mateja kilimshtua sana Bi Shuu kwani hata vizawadi navyo vilikatika. Siku moja aliniweka chini na kuniuliza.

“Manka kulikoni?’
”Hata mimi sijui.”

“Manka kila siku hujui wakati unaharibu.”

“Bi Shuu unanilaumu bure.”

“Hivi kama na huyu atakuacha unafikiri utampata nani?”

“Bi Shuu nimejitahidi kwa kila ulilonifundisha nililifanya lakini matokeo yake ndio hayo lazima kuna mkono wa mtu.”

“Manka kuna kitu gani alichokipenda Mateja hukumpa?”

“Mmh, kila kitu nimempa.”

“Kweli?”

“Kweli kabisa, nikudanganye ili iweje.”

“Sasa itakuwa nini?”

“Hata mimi sijui, huu utakuwa ni mkosi tu”

“Basi naomba kesho ukienda kazini niitie Mateja.”

“Mmh, sijui kama atakuja, lakini nitafikisha ujumbe.”

Siku ya jumatatu nilikwenda kazini kama kawaida huku nikifikilia jinsi ya kufikisha wito kwa Mateja wa kuitwa Bi shuu. Hakuwa Mateja niliyekuwa namfahamu. Ilionesha mapenzi yalikwisha kabisa. Kila alipoingia ofisini alinisalimia lakini hakuna kilichoendelea.

Nilipomuuliza alinijibu kwa kifupi “Nipo bize,” nilijikuta nikiiona kazi ngumu kama si Bi Shuu ningeacha kazi kutokana na kujiona sina thamani tena kwa Mateja. Siku moja roho iliniuma sana baada ya msichana mmoja kuingia ofisini kwa Mateja bila kumuulizia kwangu kama ilivyokuwa kwa wateja wengine.

Niliacha kazi zangu na kumfuata ndani, nilipoingia ofisini mbona  lilinishuka mtoto wa kike. Niliwakuta wamekumbatiana na Mateja huku midomo yao ikiwa imegandiana. Nilitamani ardhi ipasuke inimeze, nilisimama kama sanamu nisijue cha kufanya, machozi yalinitoka bila kizuizi, pamoja na kuniona hawakushtuka ndio kwanza walizidisha kutomasana kimahaba. Niliona wazi kabisa penzi langu na Mateja limefika ukingoni.

Nilirudi ofisini kwangu na kukaa chini kazi ilikuwa chungu nilijikuta nikilia peke yangu, nilitamani kuondoka niiache kazi. Lakini niliyakumbuka maneno ya Bi Shuu kuwa siku zote penzi tamu ni lile lisilo sukumwa ninalosukumwa lina kasoro.

Nikiwa nimeinama nafuta machozi nilishtushwa na sauti ya Mateja.

“Manka.”

Bila kuitika nilinyanyua uso kumuangalia huku kitambaa kikiwa karibu na macho kufuta machozi. Mateja alikuwa amesimama mbele ya meza yangu akiwa ameshikana kimahaba mmoja alimshika mwenzake mkono shingoni na mwanaume kiunoni.

“Vipi mbona unalia?” Mateja aliniuliza kwa kunikujeli, sikumjibu niliendelea kufuta machozi.

“Manka huyu ndiye mke wangu mtalajiwa.”

Sikumjibu niliinama chini na kulia kilio cha kwikwi ambacho Mateja na mpenzi wake hawakukijali. Niliwasikia wakiondoka, niliwasindikiza kwa macho mpaka walipotoweka, baada ya kutoweka machoni mwangu nilijikuta nikijiuliza nalia nini kwani tukio lile halikuwa la kwanza upande wangu kutendewa.

Ni kweli lazima moyo uniume kutokana na ahadi nzuri za Mateja ambazo nilijua zitanibadilisha katika maisha yangu. Ndoto yangu ya mchana ya kumiliki gari na nyumba iliyeyuka kama bonge la mafuta katika kikaango cha moto. Baada ya muda Mateja alirudi na kunipita kuingia ofisini kwake bila kunisemesha jambo lolote.

Nilikumbuka wito niliopewa na Bi Shuu wa kwenda kuzungumza naye juu ya matatizo yangu, kila nilipotaka kumwambia moyo ulisita na kuamua kuipotezea tu. Muda wa kutoka nilijikuta nikijikaza kike na kumueleza.

“Samahani bosi.”

“Bila samahani,” Mateja alinijibu kistaarabu.

“Bi Shuu alikuwa anakuita.”

“Bi shuu naye ana shida gani tena?”

“Hata sijui.”

“Mmh, yule bibi na umri wake yuko vile wakati wa usichana wake alikuwaje?”

“Mmh, sijui.”

“Basi mwambie nitamtembelea wikiendi.”

Jamani kauli ya Mateja ilinipa matumaini labda atarudisha moyo wake, siku zote nilimuamini Bi Shuu kwa maneno yake matamu yaliyojaa misemo nahau na methani ili kumlainisha mtu.

“Jamani bosi kwa nini usiende leo?”

“Manka nipo bize sana atanisamehe, lakini mwambie sijamdharau nitaitikia wito wake.”
 ITAENDELEA SIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.