DU MAKUBWA! WADADA WA BONGO MOVIE WAISHI KWA KUTEGEMEA MABWANA
Na Gladness Mallya RAIS wa
Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amempongeza
msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel baada ya hivi karibuni kuandikwa
kwenye mitandao mbalimbali kwamba sanaa hailipi hivyo wasanii wa kike
wanaishi kwa kupewa fedha na wanaume zao.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba.
Akistorisha na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema kauli hiyo aliyotoa
Aunt ni ukweli mtupu kwani kwa Tanzania sanaa hailipi hivyo wasichana
wengi wanaishi kutokana na fedha wanazopata kwa mabwana zao ndiyo maana
unakuta wanatembelea magari ya kifahari mpaka watu wanajiuliza wanapata
wapi.
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
“Alichokisema Aunt ni kweli kabisa na mimi nilishaongea sana kuhusu
wasanii wa kike kuuza sura kwa ajili ya kupata mabwana hata Steve
Nyerere alishakiri kwamba kwenye tasnia kuna wanaume wanajihusisha na
ushoga, sanaa ngumu jamani,” alisema Mwakifwamba.
CHANZO NI GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment