DANCE 100 WAPEWA SOMO NA BASATA
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akiongea na vijana
wanaoshiriki katika robofainali ya Dance 100 wakati wa semina
iliyoanandaliwa na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la
sanaa(BASATA) shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo
vikundi 16 vimeingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi
kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Washiriki
wanaoshiriki katika robofainali ya Dance 100 wakiwa katika picha ya
pamoja na majaji wa shindano hilo Queen Darleen na Super Nyamwela wakati
wa semina iliyoanandaliwa na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa
la sanaa(BASATA) shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo
vikundi 16 vimeingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi
kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Mmoja
wa Majaji wa shindano la Dance 100,Super Nyamwela akisalimiana na
washiriki wa shindano hilo walioingia robofainali wakati wa semina
iliyoanandaliwa na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la
sanaa(BASATA) shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo
vikundi 16 vimeingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi
kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Washiriki
wa shindano la Dance 100 wanaounda kundi la Wazawa crew toka Temeke
jijini Dar es Salaam wakipitia mkataba wakati wa semina iliyoanandaliwa
na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la sanaa(BASATA) shindano
hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo vikundi 16 vimeingia robo
fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi kitakachoshinda katika shindano
hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Washiriki
wa shindano la Dance 100 wanaounda kundi la Best Love toka Temeke
jijini Dar es Salaam wakipitia mkataba wakati wa semina iliyoanandaliwa
na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la sanaa(BASATA) shindano
hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo vikundi 16 vimeingia robo
fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi kitakachoshinda katika shindano
hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Waratibu
wa shindano la Dance 100 kutoka kushoto Bhoke Egina na Happy Shame
wakihakiki ujazaji wa mikataba ya washiriki wa shindano hilo wakati wa
semina iliyoanandaliwa na EastTV kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la
sanaa(BASATA) shindano hilo limedhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo
vikundi 16 vimeingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi
kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi
milioni 5.
Na Mwandishi WetuWASANII wa vikundi 16 vilivyoingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya 'Dance 100%' yaliyoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, wametakiwa kuwa wabunifu zaidi katika kucheza mitindo mbalimbali kama wanavyofanya wasanii wa nchi za nje.
Hayo yamesemwa leo/ jana na mmoja wa majaji wa shindano hilo, Hassan Mussa (Super Nyamwela) wakati wa semina iliyokuwa ikitolewa na Baraza la sanaa la Taifa(BASATA) jinsi ya kuwapiga msasa wasanii walioingia robo fainali ya mashindano hayo.
Mussa alisema ni wakati wa kila dansa kuwa mbunifu kama wanavyofanya wasanii wa nje na kuacha kung'ang'ania mtindo mmoja.
"Wasanii wenzangu inabidi twende na wakati, tujitahidi kuwa wabunifu wa mitindo badala ya kukalia tu mtindo mmoja maana kuna mitindo mingi ambapo tukiwa wabunifu tutaweza kufaidika nayo katika kutufikisha mbali zaidi katka tasnia yetu,"alisema Mussa.
Naye mratibu wa mashindano hayo, Happy Shame alisema semina hiyo imeandaliwa ili wasanii wa vikundi 16 vilivyoingia robo fainali waweza kuelezwa vigezo vinavyotumika kuwapata washindi na pia kuwafahamu majaji.
Shame alisema semina kama hiyo itakuwa ikifanyika kila hatua inayoendelea ili kuwafanya washiriki kuwa kitu kimoja na pia kuwapa uelewa zaidi wa mashindano hayo.
Alisema hatua ya robo fainali ya mashindano hayo itafanyika Agosti 23,mwaka huu kwenye ukumbi wa Don Bosco Oysterbay na washiriki wa vikundi sita wataaga rasmi huku washiriki wa vikundi 10 wakiingia nusu fainali.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema lengo la kudhamini mashindano hayo ni kwa ajili ya kuwapatia ajira vijana kupitia katika tasnia hiyo.Nkurlu alisema ni vema na makampuni mengine yakaiga mfano huo wa kuwakomboa vijana kwa kuwapatia ajira kupitia kwenye vipaji vyao.
"Ni vema tukaisapoti serikali katika suala zima la ajira kwa vijana na ndiyo maana tumeamua kudhamini mashindano haya,"alisema Nkurlu.
Naye Afisa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi aliwaasa washiriki wote kuhakikisha vikundi vyao vinasajiliwa ili kuweza kikidhi viwango vya kufanya kazi kimataifa na kudumu badala ya kuwa vikundi vya mashindano tu.
Mwisho.

Post a Comment