ad

ad

Ulinzi wa Maximo kiboko, mabaunsa 7 kazini


KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, ameonyesha uzalendo baada ya kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia pamoja na mashabiki na wanachama wa Yanga.
Maximo alihudhuria mechi ya Ufaransa dhidi ya Ujerumani ambayo ilishinda bao moja na mashabiki walijitokeza kwa wingi kwenye Ukumbi wa Quality Centre jijini Dar, ingawa kivutio zaidi kilikuwa ni ulinzi wake.
Kocha wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, akisindikizwa na mabaunsa wakati akitoka kwenye Jumba la Kibiashara la Quality Center jijini Dar es Salaam, Juzi.
Walinzi mabaunsa walioshiba hasa, wapatao saba, ndiyo walikuwa wakifanya kazi ya kumlinda Maximo kila alipokuwa akizunguka katika jengo hilo.
Hata hivyo, mabaunsa hao waliweka utaratibu mzuri wa Maximo kupiga picha na mashabiki wa Yanga waliokuwa wamejitokeza kwa wingi.
Lakini wakati mwingine ilikuwa vigumu kumfikia kutokana na ulinzi huo mkali aliokuwa amewekewa.
Yanga imetoa ofa kwa wanachama na mashabiki wa soka kwenda kuona mechi za michuano ya Kombe la Dunia kwenye ‘screen’ kubwa zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments

Powered by Blogger.