ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 15


“Kwa hiyo umeamua kunitukana.”
“Shuku sikutukani nakuambia ukweli, ungenieleza mapema ningejua niishi na wewe katika muundo gani. Lakini uongo uliweka mbele, sawa ulifanikiwa kunipata kwa gia unazo, nina imani sina deni na wewe.”

“Kwa hiyo?”
“Naomba uondoke.”
“Sawa,” Shuku alisema huku akielekea upande wa dereva na kukaa kwenye uskani bila kufunga mlango.
Lily baada ya kusema yale, aligeuka na kurudi ndani. Alipoingia ndani alikimbilia chumbani na kuanza kulia kilio cha kwikwi na kumfanya dada yake kumfuata.
“Lily unalia nini mdogo wangu?”
“Dada najuta kupoteza muda wangu kwa mwanaume suruali.”
“Kivipi?”
“Hakuna kilichobadilika, nimembana kakubali yote, unafikiri kweli yule ni mwanaume sahihi kwangu?”
“Si sahihi, kwa vile sasa hivi gharama ya maisha imepanda kila kitu kinahitaji fedha, kwa hiyo umeamuaje?”
“Nimempiga chini.”
“Kwa hiyo MJ umemfungulia moyo wako?”
“Inabidi nifanye hivyo, tena kwa malengo.”
“Na kweli mdogo wangu, sasa ondoa hasira za kijinga ili kufanikisha malengo yako. Nina imani sasa hivi MJ atakupa vitu vingi.”
“Dada wivu wa kijinga nauweka pembeni ili kufanikisha malengo yangu, nikipata magari mengine mawili na nyumba hapo nitakuwa na jeuri kama hataki kubadilika naye nampiga chini.”
“Hayo ndiyo maneno ya mwanamke mtafutaji, sasa mtaishije nyumba moja na Shuku?”
“Kila kitu MJ anajua, labda amepanga kuniweka hotelini mpaka atakapo ninunulia nyumba yangu.”
“Mdogo wangu utumie mwili na uzuri wako kuyabadili maisha yetu.”
“hilo si lakusema,” waligongeana mikono na kukumbatiana.
                             ****
Shuku baada ya kuingia kwenye gari na kujifungua kwa ndani, alitulia zaidi ya robo saa bila kufanya kitu chochote akiwa haamini kilichotokea muda mfupi.
“Hivi kweli Lily kaniacha?” Shuku  alijiuliza huku akipiga mikono kwenye uskani.
“Nani kampa siri hii? Hapana..hapana any way, wacha niondoke mpenzi siyo lazima.” Shuku aliwasha gari na kuondoka kurudi nyumbani. Alilirudisha gari kwa mshikaji wake kisha alikodi bodaboda mpaka home.
Alipofika aliingia ndani na kujifungia chumbani kwake, akiwa na mawazo mengi, kwa kuiona aibu yake ya kukaa na MJ kama ndugu ipo nje. Akili yake haikumfikiria MJ kutokana na maneno ya Lily kuonesha anamponda hata MJ.
                                     ***
Lily baada ya kupata uhakika kuwa Shuku kula kulala, pamoja na mbwembwe zote kumbe hakuwa tofauti na yeye. Wote walimtegemea mwanaume mmoja, aliamua kumpigia simu MJ. Baada ya simu ya MJ kuita ilipokelewa.
“Haloo.”
“Haloo MJ mai bebi.”
“Niambie Lily.”
“Ukweli nimeujua.”
“Kwa hiyo?”
“Sasa nimejikabizi kwako naomba usiniumize tu.”
“Nakuhakikishia wewe kuwa malkia wa moyo wangu.”
“Kama ni hivyo, nitafurahi sana.”
“Siku zote mtoto mzuri kama wewe unatakiwa umilikiwe na wanaume wenye fedha kama mimi.”
“Nimeamini, nitazidi kukupenda, kwa hiyo nije home kama kawaida?”
“Noo, bado Shuku ni rafiki yangu na sipendi nimuumize zaidi, ila nitakachikifanya kwa sasa tutakuwa tuna kutania hotelini. Baada ya muda mfupi nitakununulia jumba la kifahari hapo nitakuja kama kwangu.”
“Siyo kama kwako mpenzi, bali kwako.”
“Sawa nitakuwa nakuja kwangu.”
“Nitafurahi sana mpenzi wangu, vipi Shuku akijua?”
“Kwa sasa hawezi kujua.”
“Bebi penzi kikohozi na wanao pendana hawana siri.”
“Kwa sasa tutafanya siri, kuna fedha nitampa Shuku afanye biashara kisha kila mtu atakuwa na maisha yake, hapo hata akijua hawezi kufanya kitu.”
“Kwa hiyo leo?”
“Kwa furaha yangu, mwisho wa wiki tunaruka na ndege kwenda Arusha kula raha.”
“Wawooo mpenzi wangu, usinitie kichaa cha mapenzi.”
“Tulia mtoto mzuri ule raha, punguza mapepe.”
“MJ nitatulia kwako, naomba usinitese jamani.”
“Siwezi nakupenda sana Lily, nimeamua mpaka kuitoa siri ya rafiki yangu kipenzi kwa ajili yako, amini nakupenda.”
“Hayo ndiyo maneno, kipi kinafuata?”
“Jiandae usiku nakupitia, sasa na raha kwenda mbele.”
“Najua mpenzi wangu.”
Lily alikata simu na kuruka juu kwa furaha, alimkimbilia dada yake na kumkumbatia kwa furaha.
“Vipi mdogo wangu?”
“Yaani MJ kachanganyikiwa kusikia Shuku nimempiga chini, ameniahidi vitu vingi.”
“Isiniambie.”
“Yaani wiki ijayo Arushaaa.”
“Kufanya nini?”
“Kula maisha.”
“Unaona ulitaka kumng’angania mshika pembe kumbe mwenye ng’ombe yupo.”
“Yaani nina bahati Shuku aliisha niingiza choo cha kiume.”
“Ndo ukome kufakamia mijanaume mitapeli.”
“Basi dada akininunulia gari lingine hili nitakupa wewe.”
“Uniambie!”
“Kweli dada.”
“Mbona wavimba macho wa mtaani watanikomaa, hivi tu napewa lifti napiga mpaka honi, vipi nilimiliki yangu mwenyewe mbona wataniroga.”
“Basi habari ndiyo hiyo.”
Usiku  MJ alimpitia Lily na kwenda naye kulala hoteli mpaka siku ya pili alipomrudisha.
                                *****
Penzi la Lily na MJ liliendelea kwa siri huku Shuku akiwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea. Siku zote Lily alitaka penzi lao liwe la wazi ikiwezekana awe anakwenda pale muda wote kama alivyokuwa na Shuku.
“Bebi kwa nini nisije nyumbani mi’ sijisikii raha kila siku kulala hotelini wakati una nyumba yako?”
“Si unajua nipo na Shuku?”
“Kwa nini usimuhamishe ili nihamie hapo.”
“Nilikuwa napanga kumpa mtaji kisha tuachane.”
“Basi uza gari yangu umpe huo mtaji ili atuachie tule vyetu.”
“Nimekusikia wala usiwe na shaka kila kitu kitakwenda vizuri, fedha ya kumpa ninayo kuna vitu navikamilisha ili ahame kwa hiyari yake sitaki kumfukuza.”
“Wahi basi mpenzi nina hamu ya kuwa karibu na wewe muda wote.”
“Hakuna tatizo mpenzi.”
Wakati Lily na Mj wakifanya penzi la siri, Shuku kitendo kile kilimuumiza sana cha kumtegemea mtu na matokeo yake kudharaulika machoni mwa watu. Alichoamua kuomba fedha kwa rafiki yake ili aondoke pale na kwenda kutafuta maisha mbele ya safari ili watu wasijue maisha yake.
Akiwa amekaa na rafiki yake sebuleni Shuku alionekana mtu mwenye mawazo mengi na mnyonge toka amwagwe na Lily mwanamke aliyempenda kuliko wasichana wote aliowahi kukutana nao.
Kwa upande mwingine hakumlaumu Lily kwa vile hakumweleza ukweli. Aliamini kama akianza kuishi maisha ya kujitegemea ataweza kujipanga na kutafuta mwanamke mwingine.
“Vipi best mbona kama upo mbali?”
“Kweli.”
“Tatizo nini?”
“Aisee umaskini mbaya sana.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Nisingeadhiliwa na Lily.”
“Bado unalo hilo, achana na yule malaya  inaonekana anapenda sana fedha kuliko mapenzi.”
“Hata kama anapenda pesa, inaonekana natembea bila nguo wakati najiona nimevaa.”
“Una maana gani kusema hivyo?”
“Japo unasema mali yetu lakini siri ipo wazi kuwa mimi mpambe tu mshika pembe mwenye ng’ombe unajulikana.”
“Shuku mshikaji wangu achana na maneno ya watu, ukiwasikiliza mambo yako yatasimama yao yanakwenda.”
“Ni kweli, lakini nakuomba kitu kimoja nipe mataji nifanye biashara ili nami niishi maisha yangu mwenyewe.”
“Wazo zuri, sasa umepanga kufanya biashara gani?”
“Nimeishajipanga, we nipatie hicho kiasi.”
“Kiasi gani?”
“Milioni mbili.”
“Mbona ndogo sana.”
“Kwangu zinanitosha.”
“Nitakuongezea nitakupa kumi na ile gari dogo.”
“Nitashukuru.”
Mara simu ya MJ iliita alipoangalia ilikuwa ya Lily ambaye alikuwa na miadi naye na kwenda kwenye sherehe ya harusi ya shoga yake alikuwa inafanyika Ubungo Plaza. Hakutaka kuipokelea pale alikwenda chumbani.
“Haloo bebi.”
“Bebi upo wapi nimeishafika kitambo,” Lily alilalamika upande wa pili.
“Ooh! Sorry nilikuwa na mazungumzo na Shuku.”
“Unaona sasa, nakwambia muondoe hapo atatuharibia starehe zetu.”
“Sawa bebi nitafanya hivyo muda si mrefu.”
“Kwa hiyo?”
“Nakuja mpenzi.”
“Fanya haraka kila mtu ana mpenzi wake kasoro mimi,” Lily alisema kwa sauti ya kudeka.
“Nakuja sasa hivi mpenzi wangu.”
MJ alikata simu na kukimbilia bafuni kuoga harakaharaka na kubadili nguo kisha alipiga bonge la suti la bei mbaya na kutoka kumwahi Lily.
“Sasa best kuna sehemu nakwenda, ila masuala yako kesho nitamaliza kila kitu.”
“Mmh! Kweli mtoko wa leo si wa kawaida, hakuna tatizo we wahi, mi  sina nyendo.”
“Poa wacha niwahi,” MJ alisema huku akitoka nje na kuwacha Shuku amejilaza kwenye kochi.
                             ****
Shuku akiwa amejipumzisha chumbani kwake akiutafuta usingizi simu yake ya mkononi iliita, namba ilikuwa ngeni, aliipokea.
“Haloo.”
“Haloo Shuku, mambo?” sauti ilikuwa ya kike.
“Poa.”
“Najua hunijui, lakini kunijua si muhimu kama hili lililonifanya nikupigie simu.”
“Jambo gani?”
“Nina imani upo nyumbani sasa hivi?”
“Ndiyo.”
“Mmeagana muda si mrefu na MJ?”
“Ndiyo, kwani wewe nani?”
“Tulia basi Shuku, pupa yako itakukosesha vitu vingi.”
“Haya nakusikiliza.”
“Najua umekosana na Lily, ila mpaka sasa hujamjua mchawi wako.”
“Ni kweli.”
“Shuku, Lily bado anakupenda sana ila penzi lako limewangiwa na mtu wako wa karibu.”
“Nani?”
“Sitaki kuwa muongo ila nakuomba sasa hivi uje uone jinsi ulivyo chezewa mchezo mbaya. Shuku sifa zako nazijua lakini najua nikikuchukua itakuwa vita na Lily.”
“Naomba uniambie jina lako basi.”
“Ipo siku nitakuambia lakini leo naomba ulifanyie hili.”
“Kwa hiyo nifanyeje?”
“Njoo Ubungo Plaza kuna sherehe ya harusi. Ukifika simama karibu na maegesho ya gari nijulishe kama umefika.”
“Poa nakuja.”
Shuku alikata simu na kubadili nguo haraka kisha alitoka. Hakutaka kukodi teksi aliona atachelewa alikodi  bodaboda kuwahi eneo la tukio.
Shuku alichukua robo saa kufika Ubungo Plaza. Alipofika alimpigia simu aliyemwelekeza skendo ile, baada ya muda ilipokelewa.
“Haloo, umefika?”
“Ndiyo.”
“Sogea karibu ya paking ya magari.”
“Poa” Shuku alifanya kama alivyoelekezwa alipofika karibu ya maegesho ya gari alipiga tena simu.
“Nimefika.”
“Simama hapohapo usitoke mpaka nitakapo kwambia, hakikisha macho yako hayachezi mbali na mlango wa kutokea ukumbini.”
“Sawa.”
Shuku alitulia kama alivyoelezwa macho yake hayakucheza mbali na mlango wa kutokea ukumbini,  huku akijiuliza kuna kitu gani. Kingine kilichomchanganya kilikuwa amefuata nini pale hata kama akimuona Lily na mwanaume mwingine, hakuna na nguvu  tena kwa vile walikuwa wameisha tengana.
Lakini kauli ya aliyempigia kuwa afike pale amuone mchawi wake ndiyo iliyomfanya aendelee kuwepo.  Muda nao ulikatika na kuzidi kumfanya Shuku atamani kuondoka. Aliamua kumpigia simu kumweleza amechoka kusubiri.
Baada simu kuita kwa muda ilipokelewa.
“Haloo Shuku.”
“Vipi mbona muda unakwenda, kama bado wacha niende.”
“Nooo Shuku, vumilia kama robo saa, kila kitu kitakuwa wazi mbele ya macho yako.”
“Mmh! Sawa.”
Shuku alitulia kusubiri alichoitiwa, baada ya muda simu yake iliita, alipokea.
“Haya sasa Shuku kazi kwako kazi yangu imeishia sasa angalia mlangoni.”
Shuku alitumbua macho mlangoni aone alichoitiwa.
Kwenye mlango wa kutokea aliwaona watu wawili mwanamke na mwanaume wakitoka wakiwa wamekumbatiana kimahaba. Alituliza macho kuwaangalia baada ya sekunde chache alimgundua yule mwanaume ni rafiki yake kipenzi MJ.
Lakini mwanamke hakumwelewa kwa vile alikuwa mbali vilevile kichwa cha mwanamke kilikuwa kimelalia kifuani kwa MJ. Waliposogea karibu hakuamini macho yake kumuona MJ akiwa na zilipendwa wake Lily wakionesha ni wapenzi wa muda mrefu.
Bila kujielewa alijikuta akisogea mbele mpaka alipowakaribia karibu na kuwashuhudia wakilishana mate bila kuhofia watu waliokuwa wakitoka ndani ya ukumbi.
“Mjuniii,” Shuku alipiga ukelele kwa kulitaja jina kamili ya rafiki yake.
MJ alishtuka na kujikuta akimsukuma Lily pembeni na kumfanya aanguke chini.
“Mjuni rafiki yangu unyama gani ulionifanyia. Wanawake wote ulionao hukuridhika umeamua kuninyang’anya mpenzi wangu, kwa vile tu una pesa?” Shuku alisema kwa sauti ya kilio.
“Sa..sa..mahani Shu..shu,” MJ alisema huku akimfuata rafiki yake alipokuwa amesimama. Lakini hakufika popote Lily alijizoa pale chini alipokuwa ameanguka na kumvaa MJ.
“MJ hebu rudi, achana na mpambe nuksi mtumai mali za rafiki kumbe hana lolote,” Lily alisema huku akimvutia MJ kwake.
“Hapana Lily hebu ngoja nizungumze na Shuku najua nimemkosea.”
“MJ achana na kapuku, anapenda kula nyama wakati hana meno hebu atupishe wenye meno wajilie nyama.”
“Lily mpenzi naomba unipe dakika moja nizungumze na Shuku.”
“MJ unanipenda mimi Shuku?”
Swali lilikuwa zito kwa MJ na kujikuta akiwa njia panda asijue afanye nini. Shuku bila kusubiri, alisema kwa sauti ya kawaida.
“Mjuni nashukuru sana kwa yote uliyonifanyia, sina sababu ya kukulaumu kwa ajili ya kitendo chako cha kunidhalilisha kwa Lily.  Najua umaskini wangu ndiyo unaniponza, lakini siamini msichana uliyekuwa ukimwita malaya ndiye anayevunja urafiki wetu leo, asante,”
Shuku alisema huku akiondoka.
“Shu...shu...” MJ alijitahidi kumfuata rafiki yake, lakini Lily alimvutia kwake ili asimfuate Shuku.
Shuku hakutaka kugeuka nyuma, moyo ulimuuma alitembea huku akilia hadi kwenye kituo cha bodaboda na kukodi pikipiki.
“Niwahishe Tabata,” Shuku alisema huku akipenga makamasi mepesi.
“Elfu tatu mkubwa.”
“Poa twende.”
“Vipi kaka umefiwa?” hali ya Shuku ilimshtua dereva wa bodaboda.
“Heri ningefiwa.”
“He! Nini tena?”
“Wee acha tu.”
Dereva wa bodaboda hakutaka kuuliza zaidi, alipofika Xteno alimuuliza:
“Tabata ipi?”
“Wee umetaja bei bila kujua Tabata ipi?”
“Samahani mkubwa.”
“Mawenzi.”
Dereva alivuka barabara na kuelekea Tabata Mawenzi. Shuku alipofika alilipa anachodaiwa na kwenda ndani. Alipofika alichukua kila kilicho chake na kutimua zake kwake kurudi maskani kwake.
Aliamini maisha ya kutafuta mwenyewe yana uhuru kuliko kupewa na mtu na matokeo yake kudhalilishwa kama vile.
kwa vile alikuwa amejiimalisha kwake alirudi moja kwa moja kwenye chumba chake alichokuwa amenunua vitu vyote vya ndani kupitia fedha alizopewa na MJ.
Siku zote hakuamini maisha ya kupewa na alihofia akikosana na MJ anaweza kukosa pa kuanzia kimaisha na kuwafanya wenye mapengo wamcheke.
Kitendo cha Shuku kufumania siku ile kilimuuliza sana MJ na kupanga akirudi nyumbani amuombe msamaha kwa gharama yoyote. Aliamini akimtangazia fedha na dhiki aliyonayo atakubali tu na kumwachia Lily.
Lakini alishangaa kutomkuta nyumbani, aliondoka na mpenzi wake akiamini huenda kesho atamkuta. Siku ya pili aliporudi hakumkuta tena. Kwa vile alikuwa bize na Lily hakujua kinachoendelea nyumbani. Alimuachia Shuku fedha nyingi kitandani kwake akiamini bado yupo pale.
Wiki ilipokatika ndipo alipogundua Shuku hayupo, hata alipokwenda alipokuwa akiishi zamani aliambiwa amehama. MJ hakutaka kumtafuta aliendeleza mapenzi kwa Lily. Kwa vile MJ hakutaka kubanwa na mpenzi wake alimnunulia nyumba ili aweze kuendelea na tabia zake za kubadili wanawake kama nguo.
Mwanzo Lily alilifurahi penzi la MJ kwani muda mwingi alikuwa naye pia kila alichokitaka alikipata. Siku zote mjusi hawezi kuwa nyoka, siku moja wakiwa chumbani wanajiandaa kwa chakula cha usiku simu ya MJ iliita, alipoangalia alikuta ni mpenzi wake mtoto wa waziri aliyekuwa nje ya nchi kuonesha alikuwa amefika siku ile usiku.
“Sorry mpenzi,” MJ alisema huku akipunguza kuni kwenye jiko. 
“Ya nini tena bebii?” Lily alilalamika kwa sauti ya mtu aliyekuwa akitafuna pilipili.
“Kuna simu muhimu nataka kusikiliza mara moja.”
“Jamani bebi, utasikiliza baadaye mwenzio zipo juu zinataka kumwagika zishushe mpenziiii.”
“Samahani mpenzi ni simu ya muhimu sana.”
“Jamani, basi wahi kurudi,” Lily alisema huku akijikunja kutokana na kunyemvuliwa na wadudu wadogo wadogo.
MJ alinyanyuka na kwenda kuzungumzia sebuleni kwa sauti ya chini.
“Halooo Sweet.”
“Bebi upo wapi, mbona nyumbani haupo?”
“Nipo club.”
“Upo club gani nikufuate, nimefika usiku huu na ndege siwezi kwenda nyumbani mpaka nikuone na unipe raha zangu nilizozimisi kitambo.”
“Kwa hiyo tukutane wapi?”
“Popote, utakapotaka kama kwako nikusubiri au hotelini?”
“Nikukute Prinsess Motel.”
“Utanikuta nimechukua chumba kabisa yaani nina hamu na weeewe.”
Baada ya kukubaliana MJ alijikuta amesimama kama mnara asijue akamwambie nini Lily kwani alikuwa kwenye hali mbaya alihitaji msaada wake kumrudisha kwenye hali nzuri.
Kwa mahanjamu aliyokuwa nayo Lily, MJ alijua kama atampa huduma ya kwanza lazima angekesha na anapokwenda lazima atachelewa pia angeonekana katumika.
Alirudi hadi ndani na kwenda kwenye nguo zake na kuanza kuvaa. Lily alishtuka na kumuuliza.
“Vipi sweet mbona hivyo?”
“Aisee kuna kazi inatakiwa kufanyika usiku huu ni mimi tu niliyekuwa nimechelewa kufika.”
“Jamani mpenzi waambie wenzako muifanye kesho. “
“Bebi kazi hiyo ndiyo inatupa jeuri ya mimi na wewe kufanya yote haya.”
“Basi nipe hata chozi la mnyonge, hali ni mbaya,” Lily alilalamika alikuwa kama kachambia pilipili.
 “Bebi nachelewa wananisubiri,” MJ alisema huku akivaa haraka na kwenda kumbusu Lily aliyekuwa kwenye hali mbaya.
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA

KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
SEHEMU YA 9==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-09.html
SEHEMU YA 10 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-10.html
SEHEMU YA 11 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-11.html
SEHEMU YA 12 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-12.html
SEHEMU YA 13 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-13.html
SEHEMU YA 14 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-14.html

:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee.

Hakika si ya kukosa hii.

Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE

No comments

Powered by Blogger.