MANENO ALIYOTAMKA LUIZ FELIPE SCOLARI BAADA YA KUFUNGWA 7-1 NA UJERUMANI
Luiz Felipe Scolari, kocha wa Brazil
"Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na
siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea.
Nani anawajibika kwa matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo
haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya
kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa
chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango
chetu cha mwisho-lakini tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani.
Hatukukata tamaa na kurudi nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya
kufungwa bao la kwanza na kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani
hawawezi kuelezea ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na
unatakiwa kuheshimu hilo.
Tunatakiwa
kujiunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu wa Brazil ni
huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi kwasababu
hatujaweza kufika fainali-na tutajitahidi kushinda mechi ya nafasi ya
tatu. Bado tuna sababu ya kucheza.”

Post a Comment