TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 12
#SEHEMU ZA NYUMA ZOTE ZIPO HAPA CHINI
#HII SEHEMU NI YA JUMAPILI HII JULY 06,2014
MJ alikuwa akichemka hata kasi yake ya kupiga kasia ilikuwa ndogo tofauti na Shuku, Lily ilibidi atumie mtindo wa kujihudumia mwenyewe bila hivyo angeumbuka baada ya kumuona MJ rigwaride limemshinda.
Kwa vile walikuwa wamechoka walijilaza ili kupumzika kabla ya kupata chakula cha usiku.
****
Mambo aliyofanyiwa MJ na Lily yalipagawisha na kufikiria mara mbili kumuachia rafiki yake aendelee na yule msichana. Katika kutembea kote na wanawake hakuwahi kukutana na mwanamke anayejua kukitendea haki kitanda kama yule.
Hata alipochemsha aliendelea kula raha huku akiwa ametulia kwa mtoto kujituma muda wote. Alijua kudeka wakati pipi imo mdomoni utafikiri mtoto wa paka mwenye njaa aliyelilia maziwa.
Alijifikiria ili kumteka lazima amnunulie gari kali ili hata mwenyewe achanganyikiwe. Siku ya pili MJ na Lily walikwenda mpaka show room kuchagua gari. Baada ya kufika alimweleza Lily:
“Mtoto mrembo chagua gari utakalo”
“Nataka hilo,” Lily alichagua BMW X6 ambayo ndiyo ilikuwa bado ipo katika chati. MJ hakumung’unya maneno wala kupepesa macho, aliandika hundi na kumnunulia Lily gari la kuwatesa wanuka vikwapa na wavimba macho.
Baada ya kumnunulia waliagana na MJ na kuahidiana kuonana baada ya siku mbili.
“Jamani sweet kwa nini nisiwe na wewe tu kuliko kuendelea na Shuku?” Lily alinogewa na kumsahau Shuku.
“Hapana, jamaa kawahi sitaki kuvunja penzi lenu hasa ukizingatia sisi ni ndugu.”
“Basi naomba kila siku tuwe tunakutana basi, jamaa nitakuwa namyeyusha.”
“Hapana siyo kila siku na siku tukikutana tunachuniana ila ukishindwa unaweza kushangaa tunasitisha zoezi.”
“Zoezi gani?”
“Si kila mtu anaanza kivyake.”
“Nimekuelewa baby, usiniache nakupenda baby.”
Waliagana kila mmoja alikwenda kwake huku Lily akikanyaga mchuma wake mpya hadi kwao. Alilipaki kwao na kuteremka kila mtu alijua ameazima. Aliingia ndani kwa mbwembwe nakwenda kuutupa ufunguo wa gari kwa dada yake aliyekuwa amejilaza kwenye kochi.
“Vipi mwenzetu?” dada yake alishtuka.
“Dada, mwanamke ukijua kutumika utapata kila kitu.”
“Una maana gani?
“Dada usiku wa jana ulikuwa wa kukumbukwa.”
“Usiniambie mdogo wangu!”
“Twende nje ukaone?”
Walitoka nje na kukuta gari la kifahari, dada yake aliuliza:
“La nani?”
“Langu.”
“Muongo!”
“Kweli langu, kazi ya usiku wa leo imezaa gari hili.”
“Kumbe yule shemu ana umatemate sana?”
“Siyo yule ni ndugu yake.”
“Lilian! Mbona sikuelewi aliyekununulia ni yule mpenzi wako mpya au ndugu yake?”
“Ndugu yake.”
“Sasa ndugu yake akununulie kwa misingi ipi?”
“Dada ndiye niliye lala naye usiku wa kuamkia leo.”
“Kwa hiyo umewachanganya ndugu?”
“Ndiyo.”
“Wewee! Mbona unataka kuleta balaa?”
“Walaa, wao wenyewe, yeye anajua natembea na ndugu yake kaanza kunipa zawadi mara cheni, mara mifedha, si unakumbuka nilikueleza siji kwenye shughuli alitaka niwe naye usiku wa jana. Basi mambo niliyompa Shuku si kamweleza ndungu yake kuwa nina uwezo wa kuupanda mnazi bila kutumia mikono.”
“Mwari wee temea chini, mhu?” stori zilimpagawisha dada Lily.
“Basi mwanaume kaingia kichwa kichwa na kuniahidi gari kama nitamfurahisha kama nduguye.”
“Kama nakuona, mhu mdogo wangu lete utamu,” dada alitia chachandu ya maneno ya mdogo wake.
“Si ndiyo tukakubaliana tulale pamoja?”
“Ehe, koleza utamu.”
“Mtoto wa kike niliapa kufia kitandani ilimradi nilipate hiyo gari. Wasiwasi wangu nilijua patachimbika bila jumbe kumbe...”
“Eeh!”
“Aah! Wapi,kumbe mwepesiii, hata kiganjani hajai, mbona gari nimelipata buuuure.”
“Kivipi mdogo wangu?”
“Yaani nilivyojiandaa kumbe si lolote si chochote, nilikuwa sawa na kuburuza maiti ndani ya maji.”
“Wewee!”
“Dada alivyoonza nikaogopa nikajua mtoto wa kike naweza kukimbia na kufuri mkononi. Kila dakika zilivyokuwa zikizidi kukatika ndivyo alivyokuwa akipoteza uwezo wake. Yaani hatua za mwisho ilibidi niwe mpiga debe, konda na dereva mwenyewe.”
“Mmh! Sasa kipi kilichomfanya akununulie gari?”
“Dada wakati ana nguvu nilichokifanya hawezi kusahau hata alipochoka kama dume la bata niliendelea kumpa machejo ya kinyozi wa kipara.”
“Mdogo wangu kwa maneno, kinyozi wa kipara ndiyo machejo gani tena?”
“Dada si unajua mtu anayenyolewa kipara hatakiwi kijitikisa, akijitikisa amekatwa?”
“Ndiyo, ehe?”
“Basi, baada ya kuchoka nilimuweka mkao wa mtu anayenyolewa kipara, mtoto wa kike nikageuka kinyozi kwa kukwangua kila kilichopo kichwani na kuwa mwepesiiii.”
“Hongera mdogo wangu, sasa itakuwaje? Mmoja unampiga chini?”
“Mmh! Jamaa amekataa nisiachane na ndugu yake, eti niendelee naye penzi letu liwe la siri.”
“Mmh! Haya, kwa hiyo kadi ya gari amekupa?”
“Kila kitu dada, gari mali yangu.”
****
Kama kawaida Shuku jioni alimfuata mpenzi wake na Jeep, alipofika aliisimamisha sehemu yao ya kawaida na kupiga honi. Lily aliyekuwa amejilaza chumbani alinyanyuka na kuchukulia nje.
Alipoliona Jeep alifurahi na kujua MJ amekuja, kutokana na tamaa alijikuta mapenzi yote kayaamishia kwa MJ.
“Dada jamaa amekuja.”
“Nani?
“MJ.”
“Mbona hajakujulisha?”
“Labda kanifanyia surprise, machejo ya yana lazima angenitafuta.”
“Naona ukimpa mara tatu atakununulia ndege.”
“Wacha nimuwahi baba asije kasirika.”
Lily alisema huku akitoka nje na kwenda mbio kumlaki mpenzi wake. Alipokaribia Shuku alitoka kwenye gari na kumfanya Lily ashtuke.
“Ha! Ni wewe?”
“Ndiyo mpenzi nimeamua kubadili gani?”
“Mmh! Karibu.”
“Asante, vipi mbona kama hujajiandaa.”
“Naumwa.”
“Nini tena mpenzi ingia kwenye gari twende hospitali.”
“Nimeisha kwenda.”
“Pole sana mpenzi,” Shuku alisema huku akivuta pochi na kuhesabu wekundu ishirini na kumpa.
“Zitakusaidia kununua matunda.”
“Asante.”
Lily aliona kama Shuku anacheza lakini alizipokea na kuagana naye. Alirudi ndani ya Shuku alirudi zake nyumbani na hamu zake. Lily alipofika ndani dada yake alimuuliza.
“Vipi mbona shemu kaondoka leo hamtoki?”
“Si kaja yule mchovu nikamdanganya naumwa si kajiiiikakamuuua na kutoa vilaki viwili eti ninunue matunda.”
“Mmh! Mbona makubwa laki mbili tu ununue matunda?”
“Umeona nyingi?”
“Tena sana, kwa hiyo umeanza kumchoka?”
“Dada siwezi kutumikia mabwana wawili tena wa nyumba moja, lazima niachane na Shuku.”
“Lily..Lily mdogo wangu usiache mbachao kwa msala upitao. Kwanza hiyo mali ya nani?”
“Sijajua kila mtu ukimuuliza anasema ya wote.”
“Sasa nataka kukuambia huenda mali ni ya Shuku, siku zote mwenye fedha huwa mgumu kuliko mtumiaje asiyejua uchungu wa fedha. Kuwa makini unaweza kumuacha Shuku kumbe ndiye tajiri na huyo MJ mpambe mshika pembe tu.”
“Mmh! Kweli eeh!”
“Tumia akili, heri uende nao wote kwa siri ili Shuku asijue, hujiulizi kwa nini MJ amesema usipokwenda anavyotaka atakupiga chini unafikiri ni kwa nini?”
“Hata sijui.”
“Basi anaongopa kuharibu kwa ndugu yake ambaye ndiye mwenye mali.”
“Mmh! Dada sasa nimepata picha mali ni za Shuku.”
Lily alikubali kuendeleza penzi la siri huku akiendelea na Shuku kama kawaida.
****
Penzi la siri la MJ na Lily liliendelea bila Shuku kugundua kilichokuwa kikiendelea huku Lily akizidi kuchanganyikiwa na ofa za MJ zilikuwa tofauti na Shuku ambaye kila siku alitoa ahadi zisizo timia.
Mabadiliko ya Lily alimshtua Shuku kutokana na kuwa na dharula kila wakati tofauti na siku za nyuma kitu kilichompa wasiwasi. Aliamini aliyemnunulia lile gari ndiye aliyekuwa akimchanganya na kumfanya amuone si lolote si chochote.
Alitamani naye kuonesha makeke yake lakini alikwama kutokana na MJ kumueleza matumizi makubwa kwake yasizidi milioni mbili.
Hali ili ilimnyima uhuru na kujiona kama anacheza makida kwenye penzi lake na msichana mrembo kama Lily. Aliamua kwenda naye hivyohivyo lakini akiamini penzi lao lilikuwa limekalia kuti kavu kudondoka asingeshangaa.
Alipanga kumpiga chini baada ya kumpa penzi zito ili popote atakapokwenda ajue jamaa hana fedha lakini mapenzi anayajua. Siku aliyompigia simu Lily wakutane ndiyo ilikuwa siku ya kuonana na MJ. Aliendelea na danadana zake.
“Haloo bebi vipi leo?”
“Mmh! Leo mama kaja.”
“Sasa akija tatizo nini?”
“Sasa nitaondoka vipi na mama kaja jioni hii.”
“Bebi mbona sikuelewi.”
“Unielewi kivipi?”
“Yaani si Lily niliyemzoea, najua siku hizi unipendi.”
“Nakupenda sana wasiwasi wako tu.”
“Hapana Lily hunipendi mapenzi yetu yamekuwa kama umeme wa mgao kama hunipendi si uniambie nijue moja,” Shuku alilalamika.
“Nakupenda Shuku.”
“Si kweli najua sasa hivi una mwanaume mwingine.”
“Shuku unalalamika sana au ndo unataka kuniacha kwa kusingizia nina mwanaume mwingine?” Lily alilia wivu wa uongo.
“Si kukuacha bali sasa hivi penzi limekuwa shubiri.”
“Niamini mpenzi wangu nakupenda sana, Shuku si muda mrefu nitarudi katika hali yangu ya kawaida. Naomba univumilie mpenzi wangu.”
“Yaani hali hii ikizidi nitashindwa mimi.”
“Basi kesho nitakuja ili kukufuta machozi, hakuna mwanaume chini ya jua ninaye mpenda kama wewe hujui tu,” Lily alimpaka Shuku mafuta kwa mgongo wa chupa.
“Mmh! Sawa nimekuelewa mpenzi wangu punguza kunitesa.”
“Nikuahidi sitakuumiza tena nakupenda Shuku wangu kesho nitakuja kweli.”
Shuku aliamini kabisa Lily hakuwa na mapenzi na yeye bali alijali kitu na baada ya kununuliwa gari la kifahari mapenzi yote aliyahamishia kwa mtu aliyemnunulia gari. Moyoni bado alijiapia kufanya mapenzi ya mwisho na kumpiga chini na yeye kuishi maisha ya rafiki yake MJ ya kubadili wanawake kwa vile hakuna wa kumuumiza zaidi heat and run.
***
Usiku wa siku ile Lily alikutana na mpenzi wake MJ Sea Cliff hotel. Walichukua chumba kama ilivyo kawaida na kusaluana nguo huku Lily akipanga kujituma zaidi baada ya kupewa ahadi ya nyumba moyoni aliapa siku ile ndiyo siku ya kununuliwa nyumba.
Wakati tui linakaribia kukolea nazi na Lily kulegea kama ute wa yai kusubiri hukumu kutoka kwa Mj, simu ya MJ iliita alipoangalia ilikuwa ya demu wake mtoto wa waziri aliyekuwa nje ya nchi. Alinyanyuka na kwenda kuongelea pembeni kwa sauti ya chini:
“Bebii.”
“Bebii upo wapi?”
“Nimetoka kidogo, vipi upo wapi?”
“Ndo nakaribia kwako.”
“Umekuja lini?”
“Ndo nimetua na ndege na breki ya kwanza kwako, kesho ndo natinga home. Nimewadanganya nitatua kesho kutwa nitakaa kwako siku mbili, nina hamu ile mbaya mpenzi wangu.”
“Mmh!” MJ aliguna na kujiuliza lazima aonane na yule binti ambaye alidanganya familia yake kwa ajili yake alijua akimkimbia ataharibu kila kitu.
“Bebii mbona unaguna au hutaki nije kwako, basi nalala hotel kwa siku bili kesho ndo nakwenda home ila ilewa nisipokuona leo nitaumia vibaya. Si unajua nilitaka nikufanyie surprise.”
“Hapana bebi lazima tutaonana japo nipo mbali kidogo.”
“Basi utanikuta kwako.”
“Hakuna tatizo bebi wangu ngoja nimpigie mtu akufungulie nyumba.”
“Hakuna tatizo ndo maana nakupenda MJ wa ukwe..ehe.”
“Umeona eeeh, poa nakuja,” MJ alikata simu na kurudi kitandani Lily alipokuwa akimsubiri ili apate nyumba usiku ule kama alivyopata gari. Japo alikuwa ameahidiwa nyumba aliamini kupitia utamu wa nyonga yake mpaka kunakucha wangetoka na kwenda moja kwa moja kwenye nyumba.
Akiwa anajiandaa kumpokea MJ kwa mahaba motomoto alishangaa mwenzake kukaa kitako na kuinama mikono kichwani.
“Bebii vipi, kuna nini?”
“Kuna tatizo lazima niondoke.”
“Tatizo gani tena bebeiii?”
“Nitakueleza kesho lakini lazima niondoke.”
“Utarudi?”
“Sina uhakika sana.”
“Basi nipe kidogo mpenzi nipo kwenye hali mbaya,” Lily alilalamika kwani alikuwa amejiandaa vilivyo.
“Hapana bebii lazima niondoke.”
“Sawa nimekubali uondoke, lakini si unajua ushazipandisha nani wa kuzishusha mpenzi, nipo katika hali mbaya basi nipe hata moja la mguu wa jini.”
“Sorry mpenzi, unavyonichelewesha ndivyo unavyozidi kunifanya nisirudi kabisa.”
“Kwani unakwenda wapi?”
“Bebii si lazima kila kitu changu ukijue,” MJ alisema huku akichukua nguo zake na kuvaa. Baada ya kuvaa alimfuata Lily na kumbusu.
“Mmmwa bebi baadaye.”
MJ baada ya kumbusu alichomoa nyekundu kumi na tano na kumtupia.
“Bebi kama nisiporudi utaweka mafuta kwenye gari lako, baii.”
Lily alishindwa kumuaga kwani moyo ulikufa ganzi baada kushindwa kutimiza malengo yake. MJ hakugeuka nyuma alitoka kumuwahi demu wake mtoto wa waziri. Alimpigia simu Shuku ampokee.
****
Muda ulizidi kukatika bila MJ kutokea saa ya ukutani ilimuonesha Lily ni saa tisa za usiku akiwa macho kumsubiri. Wazo la kwenda kwa Shuku alikuwa nalo lakini alikuwa na wasiwasi wa MJ kurudi na kumkosa.
Aliamua kukomaa mpaka asubuhi huku sumu ya mahanjamu ikiwa juu bila mshushaji kutokea. Kwa tamaa ya nyumba alijikuta akisubiri mpaka saa mbili asubuhi ndipo alipoamini MJ harudi hata simu yake haikuwa hewani.
Kwa hasira aliamua kwenda kwa Shuku ili kumkata kiu hasa alivyoufahamu uwezo wa Shuku wanapopotezana muda mrefu siku wakikutana huchimbika bila jembe. Aliwasha gari lake mpaka nyumbani kwa Shuku.
Muda alipofika alikuta bado amelala baada ya kumpigia simu alimfungulia na kuingia ndani. Alipofika alijifanya amemmisi sana Shuku na kumpiga mabusu mfurulizo.
“Vipi mbona asubuhi?”
“Kwani kuna ubaya mtu kuja asubuhi kwa mpenzi wake?”
“Hiyo iliishapita.”
“Kivipi tena bebii?”
“Ndio maana nakushangaa toka upate gari umekuwa matawi ya juu.”
Kauli ile ilimtisha sana Lily na kuona kama dhamira yake haiwezi kutimia na kuondoka na hamu zake.
“Mpenzi si nilikueleza nina matatizo jamani.”
“Matatizo kwa vile umenunuliwa gari unasahau nina uwezo wa kununua magari kama hayo kama elfu moja kwa siku moja,” Shuku alijitapa.
“Si ungeninunulia mpenzi?”
“Kwa hiyo kazi yako kuhongwa siyo?”
“Basi mpenzi, lakini nilikueleza gari hili nililikataa, lakini aliyeniletea alisema nichukue. Lakini anajua kabisa nipo na wewe na sipo tayari kurudiana naye nakupenda sana Shuku,” Lily alisema huku akimchezea chuchu na kumfanya Shuku askari ashtuke kambini na kusimama imara kutoa kipigo kitakatifu kwa adui. Lily alimvutia ndani na kumtupa kitandani na kusaula nguo chache za Shuku na yeye kuzitupa za kwake pembeni. Kutokana na kushika alikuwa kama mbwa kwa chatu.
Shuku moyoni alijiapia atakachokifanya lazima Lily amkumbuke miaka mia moja itakayo kuja kwa kuamini amezidiwa uwezo hivyo alitakiwa kutumia nguvu alizipewa na Mungu ili kumfanya Lily akitoka pale awe amechanganyikiwa. Alimuweka mkao wa kuku kwa mchinjaji na kujiandaa kupitisha kisu huku Lily akimpigia kelele baada ya kuona anachelewa.
“Shuku jamani shingo umeiona mbona unachelewesha kukipitisha kisu, Shuku nichinje...nichinje Shuku mpenzi wangu shingo yangu ni halali yako. Mpenzi ukichelewa naweza kufa...chinja...chinja shuku.” Lily alilalama baada ya kuona Shuku akileta mbwembwe.
Shuku akiwa na usongo siku ile alimuona Lily kama mpya baada ya danadana ya muda mrefu, alijiapiza kumpa penzi la mwisho kisha anampiga chini kwa kujua hakuwa na uwezo wa kumnunulia gari wala nyumba aliyomuahidi.
Lily akiwa amepagawa baada sumu ya mahanjamu kumpanda kama nyoka mwenye hasira alitamani bakora tu kwa muda ule.
“Jamani Shukuu mbona unanitesa kosa langu nini mpenzi wangu?” Alilalama huku akimtazama Shuku kwa jicho la ‘nihukumu mpenzi.’
Shuku hakujibu kitu alimweka mkao wa samaki feri na mpaaji na kuanza kumpaa kwa kucha kitu kilichozidi kumuweka Lily kwenye wakati mgumu ilikuwa kama mwenye kidonda kuweka chumvi, aliweweseka kama mtu anayetaka kupandisha shetani.
“Shu..Shu..uu..Jamani kucha hazipai samaki tumia kisu unanitesa mwezio.”
Shuku baada ya kuona magamba ya samaki yamelainika na maji ndipo alipoaanza kumpaa kwa kisu taratibu na kuzidi kumchanganya Lily aliyetoka na hamu zake hotelini alipoachwa na MJ baada ya kupakwa upupu na kufungwa kamba mikono ili asijikune.
Kutokana na kuujua uwezo wa Shuku aliamini muwasho wote utaisha. Shuku alifanya penzi la kisasi kwa kutumia kikosi cha kwanza kuhakikisha anapata ushindi wa kishindo. Kutokana na koo la Lily kukauka sana matone manne ya maji yalimtosha kulegeza koo na kwenda marikiti.
“Shukuuuuuu,” Lily alipiga ukelele mmoja na kumkumbatia Shuku kwa nguvu kama nyani aliyeukumbatia mnazi baada ya kuteleza kwenye kuti la mnazi. Alitulia kwa muda kisha kuliacha yai lipasuke kwa nafasi. Baada ya kutulia kidogo sumu ikapanda tena na kutaka itolewe.
Kwa vile Shuku alikuwa na lake moyoni baada ya Lily kurudi uwanjani aliendeleza mateso bila chuki kwa kushambulia mfululizo bila kumpa nafasi na kumfanya Lily amalize maneno yote mdomoni.
“Shuku nakupenda.”
“Muongo.”
“Kweli nakupenda Shuku wangu.”
“Siamini.”
“Kweli Shuku, mbona leo tufauti na siku nyingine, umetia nini mpenzi.”
“Kawaida tu.”
“Muongo, kuna mtu ulikuwa ukimpa raha hizi.”
“Hakuna wewe tu.”
“Shuku nakupenda, lakini mpenzi umezidi ubahili ninunulia gari ili nirudishe hili.”
“Nitakununulia.”
“Lini mpenzi?”
“Nitakwambia.”
“Ja..ja..jamani Shuu..Shuu..Shuu...te..te..tee..ee na..naaa.”
Lily alitulia na kushusha pumzi ndefu, alifumbua macho kwa shida kutaka kumuona vizuri Shuku aliyekuwa amejilaza pembeni chuma kikiwa kikoli moto.
“Shuku,” alimwita kwa sauti ya kilevi huku macho yakiwa kama mtu mwenye usingizi mzito.
“Bebi naomba basi uninunulie gari nitulie na wewe.”
“Lily ni wazi penzi lako la fedha si mapenzi ya dhati.”
“Hapana bebi unafikiri nianze kutumia gari kisha leo tena kutembea kwa miguu nitauweka wapi uso wangu kwa wavimba macho wa mtaani?”
“Kwa hiyo nisivyo kununulia huwezi kuwa na mimi?”
“Nitakuwa na wewe lakini itakuwa ngumu kuwa nawe muda wote.”
“Sikiliza Lily kuna kitu nataka kukueleza ili usisumbuke.”
“Kitu gani dia?”
“Mi naona penzi letu limepoteza mwelekeo unaonaje penzi la leo ndilo liwe la mwisho?”
“Sijakuelewa unasemaa?”
“Nasema hivi kwa vile penzi lako la maslahi zaidi, mimi na wewe naona inatosha.”
“Kwa nini bebi?”
“Siwezi kuwa na mpenzi anayefanya biashara ya mwili, kama nataka dada poa wapo tena kwa bei rahisi.”
“Shukuu umefika huko?” Lily alishtushwa na kauli ya Shuku.
“Sijafika huko bali ukweli ni huo.”
“Shuku nakuahidi basi kukusikiliza kwa chochote nakupenda sana mpenzi wangu. Naomba uniache nakupenda kama nimekukosea naomba unisamehe.”
“Utanipendaje wakati sijakukununulia nyumba wala gari?”
“Shuku nakuahidi kukupenda ulivyo.”
“Lily unayoyasema ukienda kinyume wala usisumbuke kunitafuta kila mtu ashike hamsini zake.”
“Shuku mbona hivyo au umempata mpenzi mwingine?”
“Sina shida ya mwanamke mwingine, nikishikika nakwenda kwa dada poa nakata hamu zangu narudi kulala.”
“Basi mpenzi nitakufurahisha.”
“Wewe tu.”
“Basi mpenzi nipe raha zangu yaani leo uniishi hamu kila nikitulia mashetani yanapanda tena.”
Shuku kama kawaida aliendeleza makamuzi yaliyomtia wazimu Lily na kumwacha njia panda afuate kipi gari na fedha za MJ au penzi tamu la Shuku. Katika maisha yake yote toka avunje ungo hakuwa kukutana na mpaa samaki kama Shuku anayejua kumpaa na kumfanya samaki afurahie kuondolewa magamba.
Shuku aliamua kumtesa Lily kiungo cha kati alikikamata yeye na kumfanya Lily muda wote autafute mpira. Shuku hakutaka kumfunga kila alipobaki na kipa alirudisha mpira nyuma na kumfanya Lily alalamike.
“Shuku mpenzi nifunge jamani mateso gani haya yenye raha, nifunge npenzi nipumzike hapa nilipo nipo hoi. Shuku aliamua kufunga bao la Shuti la mbali lililomfanya Lily kujipita kama mkizi bila mafanikio. Bila Shuku kumdaka angeanguka vibaya.
Baada ya kuvunja yai la nne kwa moja la Shuku Lily alikuwa hajitambui kwa kuangusha usingizi mzito. Shuku Naye alijilaza pembeni yake kwani naye kutaka sifa kulimfanya achoke haraka aliopojilaza usingizi ulimchukua.
***
Walishtuka wote jioni wakiwa wamechoka na njaa kali.
“Mpenzi nasikia njaa.”
“Twende tukaoge kisha tukapate chakula.”
Walikwenda kuoga walipomaliza kuoga na kubadili nguo, Lily alitangulia kutoka na kumuacha Shuku akichukua fedha. Alitoka akiwa hana hili wala lile mbele ya macho yake alishtuka kumuona MJ akiwa amekumbatiana na msichana wakilishana denda.
Alishindwa kwenda mbele na kurudi nyuma, wakati huo Shuku alikuwa akitoka.
“Vipi hujafika mbali, nilijua umeishafika nje?”
“Mm..eeh..aah,” Lily alipata kigagaziko.
“Nini mpenzi?”
“Aah..basi.”
Shuku alipotazama mbele alimuona MJ aliwa na mpenzi wake katika penzi zito.
“Sasa dia kipi cha ajabu umekiona? Hebu twende.”
Walitoka wameshikana mikono na kuwapita huku Lily akitazama pembeni moyoni akiwa na bonge la wivu. Walipotoka nje kabla hawajaingia kwenye gari Lily alimuuliza Shuku swali la kizushi.
“Yule ndiye mke wa MJ?”
“Mke! Malaya tu.”
“Ina maana si mpenzi wake wa siku zote?”
“MJ ana mpenzi mmoja? Kila kukicha anabadili wanawake kama nguo. Huyu sijui mtoto wa kigogo alikuwa nje ya nchi nasikia kaidanganya familia yake anakuja kesho ili ale raha na MJ jana na leo kisha kesho anakwenda kwao.”
“Amefika lini?”
“Jana usiku.”
“Saa ngapi?”
ITAENDELEA KESHO HAPAHAPA
KAMA ULIKOSA SEHEMU ZA NYUMA SOMAHAPA
SOMA SEHEU YA KWANZA >>>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-01.html
SEHEMU YA 2: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-02.html
SEHEMU YA 3:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-03.html
SEHEMU YA 4:==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-04.html
SEHEMU YA 5==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-05.html
SEHEMU YA 6: ==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-06.html
SEHEMU YA 7==>www.2jiachie.com/2014/06/torojo-bamia-winga-teleza-07.htm
SEHEMU YA 8==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-08.html
SEHEMU YA 9==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-09.html
SEHEMU YA 10 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-10.html
SEHEMU YA 11 ==>www.2jiachie.com/2014/07/torojo-bamia-winga-teleza-11.html
:: SHARE nyingi na COMMENT bila kusahau LIKE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa www.facebook.com/2jiachie pekee. Hakika si ya kukosa hii.
Wanaotakiwa kusoma chombezo hili ni kuanzia +18 tu!
Hairuhusiwi kunakili. Au kutoa hata neno kuhamishia kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.
a kwenye kitabu,tamthiliya ama wall ya facebook,twitter,whatsapp na sehemu nyingine pasipo idhini ya 2JIAHIE utashitakiwa!!.

Post a Comment