LICHA YA USAJILI WA SANCHEZ …MICHAEL OWEN ASEMA ARSENAL WASAHAU NNE BORA
MICHAEL Owen anaamini Arsenal itamaliza nje ya top four msimu ujao licha ya ujio wa nyota wa Chile Alexis Sanchez kwa pauni milioni 35.
Ingawa amevutiwa na usajili wa Sanchez, lakini Owen anaendelea kushawishika kuwa Arsenal kwa mara nyingine tena itamaliza nyuma ya Chelsea, Manchester City na Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England anaamini kuwa Washika bunduki hao watamaliza pia nyuma ya Manchester United chini ya himaya mpya ya Louis Van Gaal na hivyo kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
“Kwa hakika nimevutiwa sana na usajili wa Sanchez ndani ya Arsenal,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool aliyepata pia kuzichezea Real Madrid, Newcastle na Manchester United katika maongezi yake na talkSPORT.
“Usajili wake umefanya kila mmoja aridhike. Ni mchezaji wa hali ya juu na ni hatua kubwa katika mwelekeo sahihi.
“Lakini kwa mpangilio usio rasmi, nne bora yangu kwa msimu ujao ni Chelsea, Man City, Man United na Liverpool.
“Arsenal imekosa mchezaji wa kipekee kama Thierry Henry kwa miaka kadhaa. Wambaki hatua chache nyuma.”Endelea kutembelea www.saluti5.com

Post a Comment