‘SOMETIMES’ UONGO UNAHITAJIKA KWENYE MAPENZI!
KILA kukicha kunaibuka mambo mapya. Katika ulimwengu wa mapenzi kila
siku lazima uwe mwanafunzi ili uweze kuboresha uhusiano wako. Ukiacha
ubongo wako uingize vitu vipya ni rahisi kubadilika na kuwa wa kisasa
zaidi.
Somo
la leo linashangaza kidogo lakini ni vizuri kama tukijifunza. Tumezoea
kusikia kuwa uongo ni kitu kibaya katika maisha ya mwanadamu – ni kweli.
Uongo si mzuri lakini katika uhusiano na mapenzi, wakati mwingine
unanafasi na unaboresha sana uhusiano.
Kwa kawaida uongo unakatazwa kuanzia kwenye mafundisho ya dini na hata katika jamii. Mtu muongo si mwaminifu. Hakubaliki.
Hata mwanasiasa ambaye ni muongo, wapigakura wake hawamchagui tena atakaporudi mara ya pili; kwa nini? Kwa sababu aliwaongopea.
Hiyo ni kweli kabisa, lakini hapa katika Let’s Talk About Love nataka
kukupa kitu kipya kabisa ambacho hujawahi kukipata mahali popote; uongo
mtamu!
Ndiyo! Kuna uongo mzuri tena wenye faida na utakaokusaidia kukuza
upendo wako kwa mwenzi wako. Ni suala la kukubali kujifunza tu. Karibu
darasani tujifunze...
UDANGANYIFU
Rafiki zangu, sitaki kueleweka vibaya katika hili lakini kama nilivyosema mwanzo, uongo si kitu kizuri kwenye jamii. Mtu anayedanganya hakubaliki. Kwa tafsiri ya haraka, mwongo si mwaminifu.
Rafiki zangu, sitaki kueleweka vibaya katika hili lakini kama nilivyosema mwanzo, uongo si kitu kizuri kwenye jamii. Mtu anayedanganya hakubaliki. Kwa tafsiri ya haraka, mwongo si mwaminifu.
Haaminiki kwa sababu ni rahisi kutunga mambo ambayo hayapo na
akayatengenezea mazingira yakaonekana ni ya kweli. Huyu hafai hata
kidogo. Lakini rafiki zangu, katika uhusiano upo uongo ambao unakubalika
kama nilivyosema.
Nasema unakubalika maana una lengo la kutengeneza uhusiano, kuufanya uendelee kuwa na nguvu na si kuupoteza.
Huo ndiyo uongo unaokubalika. Kabla sijaenda mbele zaidi hebu twende
tukaone kwanza tofauti ya uongo mzuri na mbaya halafu tutaendelea na
darasa letu.
UONGO MZURI
Haikubaliki hata mara moja kumdanganya mpenzi wako kuhusu taarifa zako muhimu. Nasema hivyo kwa sababu utakuta mwingine anafanya kazi mahali fulani, lakini kwa sababu ya kutaka ukubwa anadanganya kwamba anafanya kwenye taasisi fulani kubwa.

Huo ni ulimbukeni ambao hauna maana. Mweleze mwenzi wako ukweli,
ukifanya hivyo atakuwa anajua yupo na mpenzi wa namna gani. Una sababu
gani ya kumdanganya mwezi wako?
Wapo wanaodanganya wanatoka katika familia zenye uwezo mkubwa
kifedha, huku wengine wakijipachika majina ya koo maarufu ili
waheshimiwe na wapenzi wao, huo ni utumwa, mbaya zaidi kuna siku ukweli
unajulikana halafu unabaki na aibu zako.
Ndugu zangu, katika maisha ya kila siku ni vyema ukawa mkweli kwa
watu muhimu wanaokuzunguka hasa mtu ambaye unatarajia awe mwezi wa
maisha yako. Utaficha mpaka lini wakati kuna siku atagundua ukweli? Kuwa
mkweli.
UONGO MZURI
Naam! Upo uongo ambao unakubalika rafiki zangu. Unajua kuna baadhi ya mambo ukiyasema kwa usahihi kama yalivyo yanaweza kuleta athari kwenye uhusiano, ndiyo maana nimesema kwamba upo uongo unaokubalika.

Inawezekana umefanya kitu ambacho hakimpendezi mpenzi wako, ama kwa
kujua au kutokujua, lakini baada ya kuhisi labda amegundua na kukuuliza,
unakataa. Ukikubali kwa kitu ambacho hakipendi inaweza kusababisha
penzi kuvunjika.
Unabaki kuwa uongo mzuri kwa sababu kwanza una lengo la kulinda
penzi, lakini pia hauna madhara kwa mpenzi wako. Huo ndiyo uongo mzuri
ninaouzungumzia hapa.
FUNGUA ubongo wako sasa, maana muda wa kujifunza
kuhusu uhusiano na mapenzi umewadia. Huwezi kukwepa kujifunza, ukifanya
hivyo utabaki na mawazo yaleyale kila siku.
Inawezekana
kwa uelewa wako kuna mambo ambayo unayafahamu kuhusu mapenzi, lakini
kwa kuwa mdau wa kona hii, unaongeza kitu kingine kipya kila siku.
Naam! Sasa nipo tayari kuendelea na mada yetu iliyoanza wiki
iliyopita. Nazungumzia juu ya uongo wenye manufaa kwenye mapenzi. Rafiki
zangu, nilipata wakati mgumu sana kwa kupokea changamoto mbalimbali
kutoka kwa wasomaji wangu baada ya sehemu ya kwanza ya mada hii wiki
iliyopita.
Nilibadilishana mawazo na wengi kwa kadiri muda ulivyoruhusu, lakini
mwisho wa yote niliwashauri kwamba wavute subira hadi leo katika
mwendelezo wake ambapo nina majibu ya maswali yote.
Hebu sasa twende tukaone uongo ambao unakubalika na hauna madhara zaidi ya kujenga uhusiano. Rafiki zangu, kuna wakati ukweli unaweza kuharibu!
Hebu sasa twende tukaone uongo ambao unakubalika na hauna madhara zaidi ya kujenga uhusiano. Rafiki zangu, kuna wakati ukweli unaweza kuharibu!
WENZI WALIOTANGULIA
Nani amewahi kuwa mkweli kwa mpenzi wake mpya kuhusu idadi ya mapatna aliowahi kutoka nao kimapenzi?
Nani amewahi kuwa mkweli kwa mpenzi wake mpya kuhusu idadi ya mapatna aliowahi kutoka nao kimapenzi?
Hebu anza na wewe mwenyewe? Jiulize, tangu umeanza mapenzi umetoka
faragha na wanaume/wanawake wangapi? Je, upo tayari kumtajia mpenzi
wako?
Umewahi kufanya hivyo? Rafiki zangu, kati ya mambo ambayo yanaudhi
sana katika mapenzi ni pale mpenzi anapogundua kwamba mwenzi wake ni
jalala, yaani ametoka na wapenzi wengi kabla yake.
Wengi wanatamani sana kusikia kwamba wao ni wa pili au tatu, vinginevyo akutane na mwanamke ambaye bado hajaanza kabisa mambo ya mapenzi. Rafiki zangu, tuwe wakweli, kumwambia mpenzi wako kwamba umeshatoka kimapenzi na wanaume hamsini, ni sawa na kumtangazia kwamba wewe ni mhuni uliyeshindikana.

Hata kama ni kweli umetoka na idadi hiyo, akikuuliza ipunguze,
mwambie yeye ni mwanaume wako wa nne! Wa kwanza, alikutoa usichana ukiwa
mwanafunzi, baada ya hapo ukaachana naye kabisa na mapenzi.
Mwingine
ulikutana naye chuo, ukamuacha baada ya kugundua kwamba alikuwa
akipenda kukutumia tu, wa tatu ulifuma meseji ya mapenzi kwenye simu
yake ukaamua kumuacha, yeye ni wa nne!
Mwanaume huyo atajisikia fahari sana kuwa na mwanamke mwenye namba ndogo ya wanaume aliotembea nao, ingawa moyoni mwako unaujua ukweli, lakini inabidi udanganye ili kulinda penzi lako. Tupo pamoja jamani?

UGOIGOI FARAGHA
Ukiwa na mpenzi wako, si ajabu katika mazungumzo yenu ya kawaida, akakuuliza kuhusu uwezo wako wa kucheza ‘ligwaride’ muwapo faragha. Kwa bahati mbaya kuna rafiki wenye matatizo ya hapa na pale faragha.

Baadhi ya wanawake husumbuliwa na tatizo la maumivu wakati wa tendo,
kuchelewa kufika mshindo na hivyo kuachwa njiani au kupoteza hamu ya
tendo.
Wanaume wao husumbuliwa na tatizo la kufika mshindo mapema, kushindwa
kurudia tendo na kuchoka mapema wakati mwenzake akiwa bado angali
anamuhitaji.
Kimsingi matatizo makubwa hapa husababishwa na utayari wa
kisaikolojia, maandalizi duni n.k. Unapozungumza na mwenzako kuhusu
hili, hutakiwi kumpa taarifa za kweli.
Zipo athari kadha wa kadha za kuwa mkweli juu ya matatizo uliyonayo
katika eneo hili. Kubwa zaidi, unajiongezea tatizo, maana utakuwa
unaingia uwanjani ukiwa unajua kabisa kwamba mpinzani wako anajua
udhaifu wako hivyo ni rahisi kukushinda!
Matatizo ya aina hii hutibiwa zaidi na mtu mwenyewe, kugundua udhaifu
wake na kuufanyia kazi. Kama umegundua kwamba unapata maumivu wakati wa
tendo, ni wazi kwamba maandalizi si ya kutosha, dawa yake hapo ni
kutumia muda mwingi katika maandalizi kabla ya kuanza kazi yenyewe.
Kueleza tatizo lako moja kwa moja, kutamfanya mwenzako awe na mawazo,
akiamini kwamba ama hutaendana na kasi yake, hatakufurahisha au
utamuacha njiani. Kwa mtazamo huo ni rahisi sana kufikiria kuachana na
wewe ili akatafute anayeendana naye.
CREDIT: Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano.

Post a Comment