LUCY KOMBA: MIMI NI ZAO LA TYSON
MSANII nguli katika soko la filamu Bongo, Lucy Francis Komba amefunguka kuwa yeye ni zao mojawapo la hayati George Otieno Okumu ‘Tyson’.
“Mimi ni zao la Tyson, nimeanzia katika mchezo wa maigizo wa Mambo hayo uliokuwa ukirushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV na ndiyo ukawa mwanzo wangu kujulikana, asingekuwa yeye sijui ningekuwa wapi,
nitazidi kumuombea ili Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi,” alisema Lucy.
Tyson aliyefariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita mkoani Morogoro na kusafirishwa nyumbani kwao Kenya, anatarajiwa kuzikwa Jumamosi hii huko Kisumu.
Post a Comment