KHAA! KOMBA...KIMENUKA SASA SOMA HAPA
UKISIKIA khaa! Kwa tafsiri ya Lugha ya Kiswahili ina maana ya
mshangao, unachosubiri ni kuona au kusikia kinachostaajabisha ambapo leo
jina la Komba mtu anayetajwa kwa hadhi ya uheshimiwa ndilo
linalowashangaza wengi, subiri uhabarishwe.
Mheshimiwa Komba akiwa na binti wa umri sawa na mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Agnes katika hoteli maarufu iliyopo mjini Dodoma.
KOMBA ANASHANGAZA NINI?
Habari zilizolifikia Dawati la Risasi Jumamosi hivi karibuni na kusambazwa pia kwenye mitandao ya kijamii zimeweka wazi kuwa mheshimiwa mwenye picha ukurasa wa mbele ambaye gazeti hili limemtambulisha kwa jina moja (kwa sababu hakuna atakayeiona picha ya ukurasa wa mbele asimtambue), akiwa na binti wa umri sawa na mtoto wake.

Akili za kuambiwa ukichanganya na zako utabaini kuwa picha hiyo haina
maudhui ya kidugu hasa ukizingatia kuwa kiambatanisho kimeonesha pia
picha ya binti huyo mwenye mavazi yaleyale aliyojifotoa akiwa na kigogo
huyo yupo mtupu, angalia ukurasa wa kwanza usihoji sana.
KARIBU KWENYE UFAFANUZI
Ufafanuzi wa picha hiyo kwa mujibu wa mitandao ya kijamii umedai kuwa mheshimiwa huyo alipiga picha hizo na binti huyo mdogo anayetajwa kwa jina moja la Agnes na kuelezwa kuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini (jina kapuni) walikuwa kwenye hoteli maarufu iliyopo mjini Dodoma.

Aidha, udadisi umeonesha kuwa uchukuaji wa picha hizo hauoneshi
uviziaji kutokana na mapozi yalivyo jambo linalotoa taswira kwamba
huenda wawili hao waliamua.
KUCHAFUKA KWA HALI YA HEWA
Tukio hilo la aibu kubwa kwa mheshimiwa huyo limechafua hali ya hewa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo watoa taarifa na wachangiaji wamekuwa wakimkejeli kwa msemo: “Uzee mwisho Chalinze.”

“Chezea mzee wa tienitieni kwa moyo mmoja weye, ndani ya kanga moko
laki si pesa,” mtoa habari kwenye mtandao aliandika huku akiambatanisha
na picha za tukio la wawili hao ambapo baadhi ya wachangia waliandika:
“Kupenda pesa kutawamaliza, binti mdogo kama huyu na jibaba kama hili wapi na wapi?” Agnesta.
“Labda alikuwa anamfundisha siasa za kisanii, kwi kwii kwiii, aibu yake kwa wananchi wake.” Paul alimaliza kwa kicheko na kuwaonea huruma walio nyuma yake.

KOMBA MWENYEWE ANASEMAJE!
Kama ilivyo ada ya Magazeti ya Global Publishers, baada ya kupata picha hizo tata lilimtafuta mheshimiwa huyo kupitia namba zake za simu ya mkononi ambapo mahojiano yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: “Naongea na mheshimiwa...”
Komba: “Ndiyo mimi, nani?”

Risasi Jumamosi: “Mimi ni mwandishi wa Gazeti la Risasi Jumamosi hapa…” Akadikia Komba kwa haraka:
“Nilijua tu kuwa mngeandika, ninyi andikeni tu, picha zimechanganywachanganywa tu hapo halafu mnataka kuandika, muandike tu.”

Risasi Jumamosi: “Mheshimiwa mimi nataka kujua tu hii ni picha yako?”
Komba: Huyo ni mimi ndiyo, lakini huyo msichana simfahamu, watu wameungaunga tu.”
Baada majibu hayo aliendelea: “Kwanza mimi sioni tatizo, angekuwa huyo msichana na mimi tumevua nguo hapo kungekuwa na tatizo lakini hapo mimi sioni tatizo, nimevaa nguo.

Risasi Jumamosi: “Lakini kuna picha zinaonesha huyo msichana akiwa mtupu na amevaa hereni hizohizo na kanga inaonekana na imepigwa katika eneo lilelile, unasemaje?
Komba: “Lakini hapo si Global! Mnanisaidiaje, mnachotakiwa ni kunisaidia jamani.”
Risasi Jumamosi: “Kusaidiwa sawa, ila tuambie ukweli juu ya hili.”
Komba: “Mi sijui nitafanyaje katika hili, huyu msichana simjui kabisa.”
Risasi Jumamosi: “Sasa imekuwaje mnaonekana pamoja?”
Komba: “We unaonaje, zimetengenezwa au vipi….(jibu likatoka kuwa hazijatengenezwa ambapo mheshimiwa aliendelea)…

“We umesema ni nani? (anatajiwa jina, kisha Komba anaendelea)…
“Jueni namna ya kunisaidia, mahasimu wangu hao wameamua kunikaanga.” Mwisho wa mahajiano.

KUTOKA KWA MHARIRI
Saga hili bado linaendelea kuchunguzwa hasa kuhusu msichana aliyekuwa kwenye picha. Ni kwa nini walipiga na mambo mengine. Endelea kufuatilia Magazeti Pendwa ya Global Publishers.

CHANZO NI GPL
Post a Comment