Ivory Coast nje ya kombe la Dunia
Matumaini ya bara la Afrika kuwakilishwa katika
mkondo wa pili wa kombe la dunia huko Brazil yalitumbukia nyong'o Ivory
Coast iliyokuwa inahitaji sare tu ilikufuzu kwa mkondo wa pili
ikiambulia kichapo cha 2-1mikononi mwa Ugiriki.
Kufuatia ushindi huo Ugiriki ilijikatia tikiti ya mkondo wa pili ambapo sasa itachuana na Costa Rica katika mkondo wa pili
Ugiriki
ilikuwa ya kwanza kuweka wazi niya yao kupitia bao la kwanza la
Georgios Samaras kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya
mlinzi wa Ivory Coast Cheick Tiote kupeana pasi bila ya kuhakikisha
usalama wake .
Ivory Coast hata hivyo ilifunga bao la kusawazisha kupitia Wilfried Bony aliyetumia vyema pasi safi kutoka kwa Gervinho.
Ivory Coast imetupwa nje na Ugiriki
Ivory Coast itajilaumu yenyewe kwa kushindwa
kusonga mbele kwani walipata nafasi nzuri ya kufanya mashambulizi lakini
Salomon Kalou akaboronga .
Hata hivyo bao la Ushindi lilitokana na penalti
katika muda wa majeruhi baada ya Giovanni Sio kulaumiwa kwa kumtega
mshambulizi wa Celtic Georgios Samaras.
Refarii alipuliza kipenga na mshambulizi huyo
akafuma mkwaju kimiani mkwaju uliotamatisha ndoto ya Ivory Coast ya
kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza .
Ugiriki ilifuzu kama mshindi wa pili katika kundi C na hivyo sasa itakwaruzana na washindi wa kundi D Costa Rica .
Penalti ya Ugiriki iliyozima Ivory Coast
Colombia ilikamilisha mechi za makundi kwa kuiadhibu Japan 4-1 na kuweka rekodi ya kutoshindwa katika makundi.
Colombia itachuana na mshindi wa pili wa kundi D
ambaye ni Uruguay baada ya timu hiyo ya Luiz Suarez kuifungisha virago
mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia ilipoilaza 1-0.
Kutokana na kichapo hicho Italia iliungana na uingereza kama timu zilizobanduliwa nje baada ya mkondo wa kwanza .
Aidha Afrika kufikia sasa haina mwakilishi katika mkondo wa pili wa kombe

Post a Comment