CHATU MKUBWA AUAWA ARUSHA JIONI HII, AFUNGWA KITAMBAA CHENYE MANENO YA KIARABU!
Chatu akiwa ametumbukia ndani ya nyumba hiyo kupitia tundu la ukutani
Hicho ni kitambaa ambacho alikuwa amefungwa chatu huyo mkiani.
Chatu akiwa amekatwa katwa na wananchi
Chatu
wa ajabu ameuawa jijini Arusha na wananchi 'wenye hasira kali' leo
jioni. Alionekana chatu maeneo ya Sakina akiingia kwenye nyumba ya mkazi
mmoja wa eneo hilo. Wananchi walipomuona, waliogopa, wakampigia simu
mwenye nyumba ambaye wakati huo hakuwepo nyumbani. Lakini cha
kushangaza, mwenye nyumba akawaambia wasimuue kwani ni mwanae! Cha
kushangaza zaidi, chatu huyo alipoangaliwa vizuri alionekana anaburuza
karatasi nyeupe aliyokuwa amefungwa mkiani ambayo ilikuwa imeandikwa
maneno ya kiarabu ambayo hakuna aliyejua yana maana gani, hatimaye chatu
huyo ameuawa!
Post a Comment