AC MILAN YAMFUKUZA SEEDORF, INZAGHI KOCHA MPYA RASSONERI
KLABU ya AC Milan imemfukuza kocha Clarence Seedorf na kumteua Filippo Inzaghi kurithi mikoba.
Mholanzi,
Seedorf alianza kazi San Siro mwezi Januari mwaka huu, akirithi mikoba
ya Massimiliano Allegri baada ya klabu kuanza vibaya msimu huu, lakini
naye ametupiwa virago baada ya Milan kushika nafasi ya nane Serie A.
Inzaghi,
gwiji wa San Siro kama Seedorf, hajawahi kufundisha timu ya wakubwa,
lakini amepandishwa kutoka timu ya vijana ya Milan chini ya umri wa
miaka 19.
Mtu mpya: Inzaghi, pichani enzi zake akiichezea Milan ameteuliwa kuwa kocha mpya AC Milan
Taarifa
yao imesema; "AC Milan inapenda kutaarifu kwamba, kocha Clarence
Seedorf amefukuzwa, na timu ya kwanza imekabidhiwa kwa Pippo Inzaghi
hadi Juni 30, 2016,".
Kufukuzwa
kwa Seedorf, kufuatia Rais wa Milan, Silvio Berlusconi kusema Ijumaa
kwamba kiungo huyo wa zamani wa Rossoneri alichangia matokeo mabaya.
Post a Comment