NAY AFUNGUKIA TUHUMA ZA KUTISHIA KUUA
STAA wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki
‘Nay wa Mitego’ amefungukia skendo ya kumtishia kumuua mdogo wake
aitwaye Amani Shija.
“Hakuna ishu kama hiyo, kwanza Amani siyo ndugu yangu wa damu ila udugu wangu naye niliutengeneza baada ya kukutana naye Ubungo miaka minne iliyopita na akaniomba nimsaidie, bila kinyongo nilianza kuishi naye hadi leo hii anaanza kunitolea maneno kama hayo,” alifafanua Nay na kuongeza:
“Ameshindwa kujielewa lakini mimi namuachia Mungu maana kama kumsaidia nimeshamsaidia sana, nshamlipia hadi chumba zaidi ya miaka minne na nikamtimizia mahitaji yake yote, lakini wapi.”
Mapema wiki hii, Amani aliripotiwa katika gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa amemfungulia mashtaka polisi Nay wa Mitego kwa madai ametishiwa maisha.
Staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Akizungumza na gazeti hili Aprili 29 mwaka huu, Nay alisema kwamba
anasikitishwa sana na malalamiko ya Amani kwani katika maisha yake
hajawahi kumtishia mtu kumuua na hajui ni kipi ambacho kimemvuta hadi
kuanza kulalama mambo kama hayo.“Hakuna ishu kama hiyo, kwanza Amani siyo ndugu yangu wa damu ila udugu wangu naye niliutengeneza baada ya kukutana naye Ubungo miaka minne iliyopita na akaniomba nimsaidie, bila kinyongo nilianza kuishi naye hadi leo hii anaanza kunitolea maneno kama hayo,” alifafanua Nay na kuongeza:

Post a Comment