ad

ad

YOUNG KILLER ADAI MUZIKI UMEKUWA MGUMU, ‘KIPAJI SIO KIGEZO CHA KUTOBOA, NI PESA’

Msanii wa Hip Hop, Young Killer Msodoki amedai kuwa game la muziki kwasasa limekuwa gumu kutokana na ushindani wa pesa ambazo wanazitumia wasanii kuwekeza kwenye muziki wao.
Young Killer amesema kuwa muziki wa sasa kipaji sio kigezo cha kufanya vizuri, bali kinachotakiwa ni kuwa na pesa za kuweza kuendesha muziki wako.
 

“Mpaka kufika nilipo nimefanya harakati nyingi sana,nimewahi kukata tamaa kabisa kufanya muziki kwasababu nilifanya kila njia, nimezungu kwa ma presenter wa radio mbalimbali lakini wapi! mpaka nakuja kutoboa nimefanya jitihada za kutosha,” amesema rapper huyo. 

“Kwahiyo namshukuru Mungu. la kusema ukweli game la muziki ni gumu sana, sasa hivi pesa ndio inaendesha muziki wetu. Ili uwe poa unatakiwa kuwekeza sana kwenye muziki. Mimi naona itafika hatua muziki wetu utamilikiwa na watu wenye pesa, kwasababu wana uwezo wa kugharamikia muziki wao kwa pesa yoyote tofauti na kwa wasanii wachanga ambao hawana pesa za kutosha kufanya kazi zao ziwe bora. Kwahiyo unaweza ukawa na kipaji na usifanye poa. 

Sasa hivi muziki sio kipaji pekee,pesa zinahitajika sana. Ndioa maana wasanii tunahitaji kuwa na menejimenti safi ya kukuweza kukusimamia. Video yangu ya My Power nitajitahidi kuifanya iwe kitu kikubwa zaidi, kwahiyo watu wasubiri vitu vizuri.”

No comments

Powered by Blogger.