USIA WA GURUMO WAGEUZA TAREHE YA MAZISHI, SASA KUZIKWA JUMANNE …alitoa agizo: “Nikifa nisizikwe mapema, mimi ni mtu wa watu”
KIKAO cha familia ya marehemu Muhidin
Maalim Gurumo kilichoamua kuwa mazishi ni Jumatatu, kimebadili ratiba ya
mazishi na sasa atazikwa Jumane.Mwanzoni kulikuwa na mvutano mkubwa wa
siku ya mazishi baadhi wakitaka azikwe Jumatatu na wengine Jumanne.
Marehemu Muhidin
Maalim Gurumo.
Mjomba wa marehemu akasema mbele ya kikao
hicho kilichohudhuriwa pia na viongozi wa Msondo Ngoma kuwa Gurumo alitoa agizo
asizikwe haraka.
“Gurumo alisema yeye ni mtu wa watu, hivyo
akifariki asizikwe haraka ili watu wake wapate taarifa na nafasi ya kumzika,”
alisema mjomba huyo wa marehemu.
Hata hivyo mwanzoni taarifa hiyo haikupewa
nguvu na badala yake upande wa pili uliokuwa unaongozwa na mtoto wa kwanza wa
marehemu ukapitisha kuwa mazishi ni Jumatatu.
Kadri muda ulivyosonga mbele fikra mpya
zikaingia na hatimaye usia wa Gurumo ukazingatiwa (licha ya kuwa unakiuka misingi
ya kiislam) na sasa ni rasmi kuwa atazikwa Jumanne kijijini kwao Masaki
wilayani Kisarawe.
Misingi ya kiislam iko wazi kwamba mtu
anapofariki basi azikwe mapema iwezekanavyo.
Mwili wa marehemu Gurumo aliyefariki
Jumapili saa 9 alasiri, umehifadhiwa hospitali ya Muhimbili.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Makuburi jijini Dar es Salaam. ambapo msafara
wa kuelekea Masaki utaondoka saa 3 asubuhi siku ya Jumanne.
Pichani juu ni Gurumo (kushoto) enzi za
uhai wake akiteta jambo na swahiba wake Hassan Rehani Bicthuka.
Unataka niwe nakutumia stori kama hizi na kila nyingine inayonifikia? jiunge na familia ya 2jiachie.com kwenye facebook hapa LIKE PAGE YETU HAPA ==> 2JIACHIE
CREDIT: SALUTI5.COM
CREDIT: SALUTI5.COM
Post a Comment