TASWIRA ZA KITCHEN PARTY GALA JIJINI MWANZA
| Pozi la Red Carpet. |
Wanawake wa Mwanza wamepata nafasi ya kuongea na Mama Victor, Aunt
Sadaka na Getrude Mongela katika Familia Kitchen Party Gala. Shughuli
hiyo ilifanyika jana Jumamosi katika
ukumbi wa Gold Crest Hotel jijini
Mwanza.
Ukiachana na maongezi kuhusu mahusiano na masuala ya kina mama,
vilevile wanawake
walipata nafasi ya kupata huduma na ushauri wa uzazi
wa mpango, vipimo vya
saratani/kansa ya mlango wa uzazi iliyotolewa bure
na Familia kupitia PSI Tanzania.
Kwa shilingi elfu kumi tu, kina mama walipata mafunzo, vipimo, chakula pamoja na
burudani ya nguvu kutoka kwa Shaa na Mwasiti.
Post a Comment