RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KUWA KIONGOZI MWENYE MCHANGO MKUBWA ZAIDI KATIKA MAENDELEO BARANI AFRIKA KWA MWAKA 2013
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
akiongea na maafisa na wageni mbalimbali katika ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya
Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo leo April 9, 2014.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye
Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013.
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na
jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo
la heshima hiyo itatolewa jioni ya kesho, Jumatano, Aprili 9, 2014,
katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini
Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais
Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini Washington kwa
sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa
viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na
kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa
mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala
ya utawala bora.
Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali
hiyo bora ya utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea
kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa
mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa
yaliyofanywa katika sera
na mifumo ya uchumi.
na mifumo ya uchumi.
Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete
alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji wa Jarida hilo ambao
walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za jarida hilo.
Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya
wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa
maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo
yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika
uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia
uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya
uongozi wake.”
Sherehe za kesho, miongoni mwa mambo
mengine, zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini
ya uongozi wa Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na
Jumuia ya Kimataifa ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine
zenye ushawishi mkubwa katika
medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.
medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.

Post a Comment