MMILIKI WA SALUTI5 AFIWA NA MAMA YAKE
Marehemu Bi Desta Mohamed enzi za uhai wake.
Mmiliki wa mtandao wa Saluti5, Said Mdoe (kushoto) akiwa na mama yake.
MAMA mzazi wa mmiliki wa mtandao wa Saluti5, Said
Mdoe - Bi Desta Mohamed - amefariki ghafla Jumatatu ya tarehe 31/3/2014
saa 1 za jioni.Alipata homa kali Jumapili mchana, akapelekwa hospitali (IMTU) akapata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Hali yake haikuwa mbaya wala ya kutia mashaka.
Jumatatu akaamka vizuri na akashinda vizuri hadi saa 12 za jioni hali ipoanza kubadilika tena. Akafariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Msiba uko Dar es Salaam, Mbezi Beach Old Bagamoyo Road kituo cha Zena Kawawa.
Mazishi yatafanyika Jumanne 1/4/2014 saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Mbezi Beach (New Bagamoyo Road) mbele kidogo ya Masana Hospital.
2jiachie.com tunapenda kuwapa pole Said Mdoe na wafiwa wote.
INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RRAAJIUN.

Post a Comment