ad

ad

Kocha Burundi amuondoa Kavumbagu Yanga SC

Na Mohammed Mdose
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba), Niyungeko Olivier, amemtaka Didier Kavumbagu kuachana na fikra za kuendelea kubaki Yanga, badala yake atafute timu nyingine nje ya Tanzania ili aweze kuimarisha kiwango chake.
Kavumbagu kwa sasa amemaliza mkataba na Yanga lakini bado anataka kubaki katika kikosi hicho, kwani mara kadhaa akiulizwa kuhusu mustakabali wa timu gani ataichezea msimu ujao, anasema anaipa kipaumbele Yanga.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Olivier alisema Kavumbagu ni lazima aihame timu hiyo kwani kiwango chake kwa sasa ni kikubwa ukilinganisha na timu ya Yanga pamoja na Ligi Kuu Bara, hivyo kuendelea kubaki atazidi kushusha kiwango chake.
Alisema kiwango cha mchezaji huyo aliyefunga bao moja wakati Burundi ikiiangamiza Stars mabao 3-0 juzi, kipo juu sana kwa sasa na anatakiwa acheze kwenye nchi zinazolipa vizuri zaidi na timu zenye ushindani mkubwa zaidi ili apambane na hatimaye kupandisha kiwango.
 “Hapa alipofikia inabidi atafute timu nyingine kwenye ligi yenye ushindani, kama akiendelea kubaki hapahapa, hakika hataweza kuendelea kwa sababu anakosa changamoto kwenye timu yake pamoja na kwenye ligi,” alisema Olivier.

No comments

Powered by Blogger.