GAZETI LA MAWIO KIKAANGONI
Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na
kukejeli nia njema ya
serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano.
Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema
gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu,
kukanusha taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23,
mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa husika
inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.
Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20
waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo shaka
kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,” alisema.
Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua
kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.

Post a Comment