CHOMBEZO: MPANGAJI SEHEMU 22 ...MWISHO
Nilikuja
kushtuka ghafla baada ya gari kupiga breki kali zilizofanya hata watu wengine
mle kwenye basi kupiga kelele za hofu na hamaniko.
“Huyu dereva
mshenzi nini.Anataka atuue wengine hapa?”.Aliongea mama mmoja mwenye mimba
baada ya breki ile.
“Hamna
mama.Kuna gari limekuja mbele ya basi letu na kumwomba dereva asimamishe na ndo
maana imekuwa ghafla hivi”.Aliongea jamaa mmoja ambaye alikuwa amekaa
dirishani.
Hadi hapo
mimi nilihisi kama nataka kufa,lakini haikuwa hivyo.Nikatamani labda niwe
ndotoni hivi,kisha nikafumba macho ili nione kama itakuwa ndoto.
Lakini
nilipofumbua,nilisikia yule jamaa anasema kuna majamaa watatu pamoja na
Mchungaji wameshuka na wanaongea na dereva.
Hapo sasa
ndipo nilitaka hata kujitupa nje kupitia dirishani kisha nikimbie kwa nguvu
zangu zote hadi sehemu ilipo salama.Lakini nilipoangalia nje,dah! Sijui hata
tulikuwa wapi maana kulikuwa ni pori tupu.
Dakika
kadhaa baadaye,niliona hao majamaa watatu wameingia mle ndani huku wamekamata
picha mkononi.
Walipotua
macho yao kwangu tu! Wala walikuwa hawana haja ya kuendelea hadi siti ya
mwisho. Wakaja kwangu na kuniamuru ninyanyuke,nami nikatii. Wakataka nitoe na
mizigo yangu yote.
Bila zengwe
nikatii huku sasa lile tumbo la haja kubwa,likirudi katika hali ile ya mwanzo..
Baada ya
kushusha mizigo yangu,waliniongoza moja kwa moja hadi kwenye Pajero waliyokuja
nayo.Mizigo wakaitupia kwa nyuma,ma mimi wakaniweka kati huku Baba Sheila akiwa
upande ule mwingine usawa wa dereva.
Safari ya
kwenda nisipo-pajua ikaanza.
**********
ENJOY.
Hakuna
aliyemsemesha mwenzake hadi pale tulipofika.
Kulikuwa
kama ni kambi hivi ya jeshi au tuseme labda ya wakimbizi,au sijui niseme
vipi.Kwani wapo waliokuwa wamekaa na wapo ambao walikuwa wanalinda usalama.
Baada ya
kuingia pale ndani.Nikatolewa nje ya gari na moja kwa moja nikaanza kupelekwa
kwenye jengo moja ambalo sifahamu hadi
leo lipo wapi na ni la nani.
Baba Sheila
akiwa mbele,mimi na wale jamaa watatu tukiwa nyuma,tuliingia ndani ya jengo
lile ambalo lilikuwa kama meli ya kivita hivi au nyambizi,zile meli za kivita
zinazozamia kwenye bahari.
“Kijana
umeingia sehemu mbaya sana.Heri ungeendelea na yule mwingine.Yule hata ungempa
UKIMWI,kwangu si kitu.Alishanitoka moyoni.Ila huyu,aisee sikuachi”.Aliongea
Baba Sheila baada ya kuingia chumba kimoja kilichokuwa na mitambo
mingi-mingi,sijui hata ya nini.
Baada ya
kuongea hayo,nilishtukia nguo zangu hasa tisheti ikivutwa kwa hasira na
kuchanwa na wale jamaa.Kisha wakaja
kwenye jinzi langu nalo wakalivua kwa hasira.Nikabaki na kikaptula cha
maua maua na singlend,ambavyo navyo vikanyofolewa pamoja na boxer langu la Man
United.
Mzee aliwaoneshea ishara wale jamaa kwa kidole.Na
wao wakatii kwa kunipeleka sehemu moja ambayo ilikuwa kama ina
senyenge.Wakanifunga pingu hapo kwa kunining’iniza huku mgongo wangu ukigusa
zile senyenge.Baada ya hapo,wakaamuriwa waondoke wale jamaa.
Vya watu
shida nyie.Mateso niliyopokea pale,nilisema nikitoka mzima,MUNGU atakuwa ngome
yangu daima.Niliapa kuwa nitamrudia MUNGU na kuwa mfuasi wake.
Ile senyenge
iliungwa kwenye umeme.Yaani pale wale jamaa walivyotoka,Baba Sheila alikuwa
anabofya sehemu moja na kufungua kidude flani hivi kimeandikwa namba.Nadhani ni
mita ya kupimia umeme.
Alipofungua
kile kidude alisababisha zile senyenge kunipiga shoti mgongoni. Pale
nilipolia,yeye alisema hata mwanangu atalia vivyo hivyo wakati anajifungua toto
lako. Hapo alizidisha nguvu ya umeme na kuwa juu zaidi ya mara ya kwanza.
Kama haja
kubwa na ndogo,zote zilitoka pale.Kilichofuata ni mimi kufumba macho
nikigugumia kwa maumivu jambo lililiosababisha nipoteze fahamu.
************
Naweza
kusema, kupoteza fahamu ilikuwa pona yangu
kwenye ule umeme.Lakini haikuwa pona ya mateso yangu.
Baridi isiyo
kifani,ilikuwa imenishika hadi nikazinduka.Nilipoangalia,nilikuwa nipo sehemu
moja kama swimming pool,lakini ndani yake kulikuwa na maji ya baridi hadi
yanatoa mvuke.
Na kila
baada ya dakika kumi,wanaweka barafu karibu ndoo sita za rita
ishirini.Niliambiwa nitakesha humo kwenye baridi kama Sheila atakavyokesha na
mimba yangu mtaani usiku na mchana akitafuta pa kujihifadhi.
Maswali
mengi mengi nikajiuliza juu ya maneno yale.Kwanza nilijiuliza kwa nini Mzee
yule alisema nitakesha kama Sheila atakavyokesha na mimba yangu mtaani.Ina
maana Sheila katoroka kwao au huyu mzee kamfukuza aende huko mtaani.
Nilibaki na
maswali hayo ambayo sikupata jibu lolote hadi leo.
Kama kupiga
kelele za kuomba wanisamehe,nilizipiga sana.Na kama kulia nililia sana ili
wanitoe mle kwenye swimming pool la mateso ya baridi.
Mwisho wa
siku pumzi ilinikwisha baada ya muda mrefu wa mimi kukaa mle kwenye
mibarafu.Miguu ikashindwa hata kusogea.Midomo ikabaki wazi na mikono
nayo,ikakakamaa. Hapo napo niliona kama kuzimu kunaniita.
Wakanitoa
kabla sijapoteza fahamu.Wakati huo ilikuwa mida ya saa mbili za usiku.
Nikapelekwa
kwenye chumba kimoja ambacho mwanzoni nilihisi faraja kuingia mle.Kilikuwa kina
joto balaa,lakini kwa kuwa nilikuwa nimeshikwa na baridi,niliona afadhari
kuwemo mle.
Nusu saa
mbele,nilianza kuona kero la joto lile.Na nilizidi kuona kero baada ya ubaridi
ule kunitoka mwilini kabisa.Sasa jasho likavaa ngozi yangu,na kama kuwiva,sasa
nilikuwa na wiva haswaa. Hapo spika za chumba kile nilisikia zikisema,eti
navyojisikia joto lile, ndivyo na Sheila atakavyojisikia wakati jua
litakapokuwa linamuishia mwilini kutafuta chakula.
Mateso yalizidi kiwango,na kama
kunyooka,nilinyooka sana kwa muda ule mchache.Nikazimia tena kamanda.
**********
Nilipozinduka
ilikuwa ni asubuhi katika chumba kimoja kidogo sana.Ilikuwa ni faraja kwani
hakikuwa na mateso kama ya jana yake.
Lakini
baadae,walikuja jamaa wengine wawili na kuanza kunibana mbavu na zaidi
waliporidhika na zoezi lile,wakachukua virungu fulani vya chuma na kuanza
kunigonga kwenye ugoko na kwenye vile vinundu ambavyo ndivyo viungio vya miguu
yangu .Hapo nilikuwa si mtu tena,bali mfu.Yale maumivu,kamwe siwezi kuyasahau
na siyafananishi na maumivu yeyote katika maisha haya.
**********
Wiki nzima
nilikaa nateswa pale,mateso ya kila aina,hadi kugalagazwa kwenye siafu. Na saa
nyingine baada ya mateso wanakuletea mwanamke wanakwambia mpe mimba
huyo,ukishindwa hata kusimamisha kichapo kinaendelea.Sikuweza zoezi lao hata
moja,hivyo mateso kwangu yakawa ni kama chakula tu!.
Mwisho
kabisa Mzee yule alisema anataka nisikie maumivu kama ambayo atayasikia mwanaye
wakati anajifungua.Hapo alisema anataka amkate P wangu.
Daah! Kama
kuomba msamaha ingekuwa ajira,mimi ningekuwa nalipwa mshahara mkubwa sana.
Niliomba
msamaha hadi ulimi ukakosa mate nikabaki kukaa na kusubiri wafanye watakacho
kwani nilikuwa sina uwezo wakukurupuka na kupambana nao.
“Sasa chagua
moja.Tuchome haya mavyeti yako ya elimu uliyotafuta miaka sijui kumi na mbili
au tukate huyo anayekupa kiburi”.Baba Shei aliniuliza.
Kwa wakati ule,vyeti
vilikuwa si kitu.Ila hii kitu bwana muhimu.Niliwaomba wachome tu!Na bila kusita
mbele ya macho yangu,nilishuhudia vyeti vikichomwa moto.
Mwisho
kabisa,waliniminya sehemu ya shingoni ambayo ina mshipa mkubwa wa damu.Hapo
nikapoteza fahamu.
*********
Nilipozinduka
nilikuwa Morogoro tena nyumbani huku kaka yangu yule wa Arusha ikisemekana
ndiye aliyenileta lakini aliondoka na kuacha ujumbe ulionipa pole lakini
ukinitaka nisiwasiliane naye tena,yaani alikuwa kachukia.
Ni wiki moja
lakini kwangu ilikuwa kama miaka.Sikuamini kama nimetoka salama.Nilimshukuru
MUNGU japo ndugu yangu aliamua kunitenga.Najua ilikuwa ni hasira tu! Na mimi
nimemsamehe kama alivyonisamehe.
Pale
nyumbani,Stela na shangazi yake walikuwepo lakini Maimuna hakuwepo.
Nilipomuulizia,walisema aliondoka baada ya kujigundua ana mimba,na mhusika
nilikuwa ni mimi.Hawakusita kusema kuwa natafutwa sana baba yake.Hapo nikazidi
pia kupagawa.
Mwezi
ukakata na hali yangu ikatengamaa tayari kwa pirikapirika za maisha.
Hakuna
aliyenijali kama hapo mwanzo.Kitendo nilichokionesha kwa kaka yangu kule
Arusha,wengi kiliwagadhabisha hasa baada ya Mzee yule kumfukuza kaka nyumbani.
Nashukuru kuwa mzee yule hakumdhuru kaka.Hiyo ni sababu kaka naye alikuwa ni
mtu wa usalama kama mzee yule,fununu hizo nilizipata kwa baba yetu.
Huyo Stela
alikuwa kabadilika sana.Tabia za umalaya ndo zikawa zake.Shangazi yake alisema
kamshindwa. Mbaya zaidi akawa ananitaka kimapenzi na wakati mwenzake sina hamu
tena na hiyo kitu.
**********
Nilitoka
pale Morogoro na moja kwa moja nikaenda
Kondoa kwa Maimuna kwa kutumia ramani niliyopewa na Shangazi wa Stella.
Nilipofika
nilipiga magoti na kuomba msamaha kwa wazazi wa Maimuna huku nikiahidi matunzo
na kumchukua Maimuna baada ya mambo yangu kukaa vizuri.
Mimba yake
ilikuwa tayari kubwa na kwa kuwa baba nilikuwa mimi,hawakuwa na
kipingamizi.Msamaha ukapita.
Baadae
niliamua kusomea udereva.Nilipomaliza nikatafuta reseni ambayo ilinifanya niajiriwe kwenye kampuni
moja ya usafirishaji ambayo hadi leo nipo huko.
Mambo
yalipokaa vizuri,nilimchukua Maimuna na kuanza kuishi naye tukiwa na mtoto wetu
mmoja.Lakini baadaye tuliongezewa mwingine na Sheila ambaye alimbwaga mtoto
yule siku moja asubuhi sana.Aliacha ujumbe tu! Wa karatasi kuwa yeye ndiye
kamleta mtoto yule.
********
Maisha
yakawa hivyo. Miaka sasa imepita tangu mkasa huu utokee. Sasa hivi nina watoto
watatu,lakini ile tabia,imenitokea puani.
Sasa
nimeokoka,na maisha yangu nimemkabidhi MUNGU.Namshukuru Mai,japo alikuwa
Muislam lakini alikubali kufunga ndoa ya bomani ambayo ndio hadi sasa inadumu.
**********
Naamini
mmejifunza mengi katika kuridhishana kimapenzi,kujikinga na
magonjwa,kuwaheshimu wale wanaojiuza na kuwaona kama hawakupenda kuwa vile.Pia
nadhani umejifunza kuwa cha mtu mavi na siku za mwizi ni 40.Mateso
niliyoyapata,siwezi kuyasahau.
Chungeni
sana vijana.
MWISHO.
Asanteni kwa
sapoti yenu.
Komenti
chochote kuhusu hadithi hii,usisite kukosoa.
Unataka niwe nakutumia stori kama hizi na kila nyingine inayonifikia? jiunge na familia ya 2jiachie.com kwenye facebook hapa LIKE PAGE YETU HAPA ==> 2JIACHIE
wazo zuri na funzo kwa sisi vijana tunaependa chini
ReplyDeleteNimeipenda!
ReplyDeleteDuh, nimepata fundisho kutokana na simulizi yako hii kali na ya kusisimua. Ahsante sana
ReplyDeleteDuh, hakika nimepata fundisho kutokana na kisa hiki cha kusisimua. Ahsante sana kwa simulizi kali kiasi hiki.
ReplyDelete