AZIZA WA FACEBOOK SEHEMU YA O4
Na Nyemo Chilongani.
ILIPOISHIA
MIMI: Duh! Wewe noma. Ndani ya wiki moja umetembea mikoa
mitatu. Big Up mkuu.
SOLO: Kutafuta kaka. Maisha kutafuta. Si unamuona hata
Ndimanga Hassan, anatembea zaidi ya mikoa kumi kwa mwezi, hatutakiwi kukaa
sehemu moja. Hadithi imeishia wapi?
MIMI: Ipi? Zipo nyingi tu.
SOLO: Ile ya yule msichana mwimbaji wa kwaya aliyekuwa
amepanga mauaji kwa mvulana ambaye alikuwa amemkataa kanisani na kuamua kutaka kumuua
nchini Zambia.
MIMI: Bila shaka unaizungumzia HER HIDDEN FACE, si ndio?
SOLO: Yeah!
MIMI: Ile ipo sehemu ya tano. Inaendelea kama kawa.
SOLO: Basi poa. Ngoja niitafute niendelee kuisoma.
EDUADO: Kaka
MIMI: Niambie kijana.
EDUADO: Mtoto leo kaja chuo aisee kapendezaje!
MIMI: Acha utani.
EDUADO: Sure. Mtoto ni noma kaka. Mtoto mrembo mpaka
anajishangaa. Namuona hewani, ushatupia mambo?
MIMI: Hapana. Nangoja anianze, asiponianza nampotezea tu kwani
si lazima kivile kuchati nae na kumshobokea.
EDUADO: Ila kaka fanya mambo bhana. Huyu mrembo sitaki umkose
kabisa.
MIMI: Usijali kaka. Huyu mdogo mdogo mwisho wa siku utamkuta
gheto kapumzika. Chezea Tandale wewe.
EDUADO: Hahaha!
AZIZA: Mambo!
MIMIl Mabaya.
AZIZA: Ubaya wake?
MIMI: Naumwa.
AZIZA: Nini tena jamani?
MIMI: Maralia. Yaani mbu mmoja tu jana chumbani kwangu ndio
alisababisha majanga yote haya.
AZIZA: umekunywa dawa?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Kwa nini sasa jamani?
MIMI: Naogopa sana dawa Aziza. Labda uje uninyweshe kinguvu.
AZIZA: Dah! Pole sana Ibra. Nitakuombea kwa Mungu akuponye.
MIMI: Asante sana. Nitafurahi sana.
AZIZA: Aya nishakushtua. Hebu niambie kuhusu vitu ulivyokuwa
ukiniambia.
MIMI: Tatizo lako unajiamini sana Aziza halafu unafanya makosa
sana kila unapoona kwamba fedha ndio kila kitu. Yaani haujifikirii kama kuna
watoto wa matajiri ambao wanaumwa sana mpaka wanakufa, kama fedha ni kila kitu
si wangepona.
AZIZA: Nafahamu.
MIMI: Basi kama unafahamu, fahamu pia kuna kitu ambacho ni
kila kitu na si fedha kama unavyofikiria.
AZIZA: Kipi tena.
MIMI: Mungu ndiye kila kitu katika maisha yetu. Bila Mungu,
huwezi kuwa na furaha hata kama una fedha, bila Mungu huwezi kupona ugonjwa
wako hata kama una fedha na kutibiwa na madaktari wakubwa duniani. Umenipata?
AZIZA: Ndio nimekupata.
MIMI: Au hadi hapo unataka kubishana tena?
AZIZA: Hapana. Ila unaonekana kuwa na hekima sana Ibra.
MIMI: Yeah! Unajua wakati mwingine yatupasa kuutambua ukweli.
Hatutakiwi kuamini sana katika fedha. Ila achana na hayo. Wewe ni mama wa
nyumbani, mwanafunzi wa sekondari au mwanafunzi wa chuo?
AZIZA: Naonekaje?
MIMI: Profile picha yako ni ya mdoli, sasa nitajua
unaonekanaje?
AZIZA: Hahaha! Usijali. Mimi ni mwanachuo.
MIMI: Unasoma wapi?
AZIZA: Mlimani
MIMI: Unasomea nini?
AZIZA: Sheria.
MIMI: Afadhali.
AZIZA: Afadhali ya nini tena?
MIMI: Uje kuwa mwanasheria wangu baadae katika kampuni yangu.
AZIZA: Hahahah! Utaweza kunilipa?
MIMI: Kwa nini nisiweze? Nitakuwa na fedha
mbayaaaaaaa....nitamiliki magari ya kifahari na majumba makubwa sana....lol
AZIZA: Yote ni mipango ya Mungu ila napenda ulivyoongea kwa
sababu unaonekana una imani ya kupata hivyo, cha msingi yakupasa kujituma tu na
kumtanguliza Allah kwa kila kitu. Naomba nikuulize swali.
MIMI: Usijali. Uliza.
AZIZA: Unaishi wapi?
MIMI: Tandale kwa Mtogole.
AZIZA: Kule kwenye wezi wengi na wakabaji?
MIMI: Si wezi wengi tu, kule kunapodharaulika na watu wenye
fedha kama nyie.
AZIZA: Hahaha! Usiseme hivyo bwana. Ila mbona umedanganya?
MIMI: Nimedanganya nini?
AZIZA: Kwenye profile lako. Umeandika unaishi Romania. Ulikuwa
unataka kujipaisha nini upate wanawake?
MIMI: Hapana Aziza. Hiyo imekuja yenyewe tu.
AZIZA: Kivipi?
MIMI: Nilikuwa nataka kupatambulisha kama home kwetu ni
Tandale. Ila nilipokuwa nikiandika Tandale, haikuwa ikitambulika kama
ilivyokuwa sehemu nyingine. Matokeo yao wao kama facebook wakaniletea Tandalesti
mji fulani kutoka Romania, nikaona sio kesi, nikakubaliana nao, ila ukiangalia
kwa makini, Tandale imetokeza katika jina hilo.
AZIZA: Yeah! Nimeona. Hebu naomba uniambie mengi kuhusu
Tandale.
MIMI: Kama yapi unataka kufahamu?
AZIZA: Mazingira, watu wa huko na mambo mengine.
MIMI: Tandale kama Tandale mazingira yake mazuri sana, watu
full kuyafurahia maisha kama kawa. Kuna watoto wazuri, watoto ambao
wanajitambua wao ni nani na kipi cha kufanya maishani mwao. Kuna mambo ya Rusha
Roho usiku, yaani kwa kifupi kuhusu maisha, huku tunakula sana bata kuliko
kwenu pa kulala saa moja.
AZIZA: Hahaha! Kwani huko kwenu huwa mnalala saa ngapi?
MIMI: Huwa nikiwa mgonjwa sana, nawahi kulala kama saa saba
hivi.
AZIZA: Saa saba?
MIMI: Yeah! Ila nikiwa si mgonjwa, mpaka adhana iadhiniwe.
Watu tunatransform usiku kuwa mchana na maisha yanasonga.
AZIZA: U must be kidding me Ibra.
MIMI: Huo ndio ukweli Aziza. Siwezi kukutania.
Unaona jinsi mawasiliano yetu yalivyokuwa yakienda? Hapo ndipo
nilipokuwa napataka sasa. Nilikuwa namletea sana ucheshi lakini mwisho wa siku
kuna kitu nilikuwa nakihitaji kutoka kwake, namba ya simu tu. Unajua katika
maisha ya kuchati facebook huwa yanachosha sana, kuna kipindi fulani
automatically unatokea kummisi mtu fulani na ungependa sana awe hewani lakini
hayupo hewani, unapokuwa na namba ya simu, inakupa wakati mzuri wa kumsikia na
kumjulia hali katika kipindi chochote ambacho ungependa kumsikia.
Ucheshi ndio ulikuwa kawaida yangu ila katika kipindi hiki
nilikuwa nataka kuuleta ucheshi mpaka katika maandishi. Aziza akaonekana
kulifurahia hilo, akaonekana kuanza kunikubali japokuwa hatujawahi kuonana hata
siku moja. Nilikuwa bize na chatting na Aziza, sikutaka kuwasiliana na mtu
mwingine katika kipindi hicho japokuwa nilimuona Eduado, Ibra Akilimia na
Emmanuel Solo walikuwa wamenitumia meseji.
Nilikuwa nikijitahidi sana kumuingiza Aziza kwenye himaya
yangu, yaani aingie bila kupenda na mwisho wa siku kila kitu kiwe poa sana.
Sikujali alikuwa akiishi wapi, sikujali na mimi nilikuwa nikiishi wapi, kitu
ambacho nilikuwa nikikiamini ni kwamba mapenzi wala hayakuwa na hiyana,
yalikuwa hayabagui watu kama tulivyo wanadamu.
AZIZA: Nikuulize kitu.
MIMI: Niulize tu.
AZIZA: Unasoma?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Unafanya kazi?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Sasa unafanya nini?
MIMI: Nipo nipo nyumbani. Nilisoma kidato cha kwanza, sikuwa
na fedha za kuniendesha kielimu, nikaachana nayo mpaka sasa hivi. Kuna kipindi
nilipata vijisenti mara baada ya kubeba sana mizigo Tandale sokoni, nikaenda
kusoma English Course.
AZIZA: Kwa hiyo haufanyi kazi?
MIMI: Yeah! Sifanyi kazi.
AZIZA: Unafanya kitu gani kingine?
MIMI: Sifanyi chochote kile.
AZIZA: Ila niliona kama unaandika hadithi! Au majina
yamefanana?
MIMI: Yeah! Huwa ninazipost tu.
AZIZA: Hadithi zile huwa unaandika wewe?
MIMI: Hapana.
AZIZA: Sasa huwa anaandika nani?
MIMI: Anaandika baba na kisha mimi kuzichukua na kuziweka
facebook.
AZIZA: Unanidanganya Ibra.
MIMI: Nikudanganye ili iweje? Kuna tuzo ya uongo wanapewa
waongo? Huo ndio ukweli.
AZIZA: Mmmh! Basi mpe hongera baba yako.
Mimi: Zimefika.
Wakati mwingine haitakiwi kuwa mkweli kwa kila kitu. Tayari
nilikwishaona kwamba kagundua kwamba sisi ni watu tunaoishi sehemu mbili
tofauti, madaraja mawili tofauti na katika kichwa chake aliamini kwamba Tandale
wanaishi watu masikini japo haikuwa hivyo. Nilichokuwa nikikifanya ni kuendana
na akili yake alivyokuwa ameiweka, nami nikaanza kujifanya masikini ambaye
sikubahatika kusoma kwa kuwa sikuwa na fedha ya kuniendeleza kielimu.
Nikafanikiwa, kwa kiasi fulani aina ya maisha ambayo nilimpa yalimfanya kuamini
kwamba kweli nilikuwa mtoto wa uswahilini, nilijivunia kuishi Tandale katika
uwepo wake.
Maisha
yalikuwa yakiendelea kama kawaida, kuhusu Aziza, wala sikuwa na wasiwasi kwa
kuamini kwamba piga ua huyu mtoto ni lazima ningemchukua bila tatizo lolote
lile. Kila siku nilikuwa nikiwasiliana nae, alikuwa akionekana kunikubali sana,
chatting zangu zilizokuwa zikitabasamu zikaonekana kuuteka moyo wake. Nilikuwa
na marafiki wengi facebook lakini nikikaa bila kuchati na Aziza sikuwa
nikijisikia furaha kabisa.
Japokuwa
Eduado alikuwa amenipa ishu ya kumfuatilia Aziza kama mchezo fulani lakini
kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo nami nikazidi
kufall inlove. Nilikuwa nikipenda sana Aziza, kila nilipokuwa nikiingia
facebook na kumkosa, sikuwa nikijisikia raha kabisa.
Kuna
nyakati za shida zikaingia, nyakati ambazo sikuweza kumuona Aziza hewani.
Katika nyakati hizo maisha yalikuwa ya tabu sana, nilikuwa nikikosa furaha hata
katika maisha ya kawaida. Nilimzoea sana Aziza, nilimpenda sana Aziza kwa hiyo
kutokuuona uwepo wake machoni mwangu kilikuwa ni kitu ambacho kiliniumiza sana.
MIMI:
Eduado vipi?
EDUADO:
Poa. Inakuwaje?
MIMI: Kama
kawa. Mbona Aziza simuoni siku hizi?
EDUADO:
Tupo kwenye mitihani kaka.
MIMI: Sasa
mkiwa kwenye mitihani ndio haruhusiwi kuwa hewani? Mbona wewe upo?
EDUADO:
Mimi si unajua mbishi kaka.
MIMI: Dah!
Nimemmisi sana Aziza. Nimemmisi ile mbaya kaka.
EDUADO:
Usijali kaka. Mitihani ikiisha atakurudi hewani tu.
MIMI: Poa.
Ila mnamaliza lini?
EDUADO:
Wiki ijayo.
MIMI: Duh!
EDUADO:
Nini tena kaka?
MIMI:
Nahisi kama nitakufa kwa mawazo. Nahisi nitaweza kufa kaka.
EDUADO:
Usijali kaka. Wewe vumilia tu utakula mbivu.
MIMI: Poa
kaka.
Katika
kipindi hicho ndicho nikajua kwamba moyo wangu ulikuwa ukimpenda sana Aziza.
Huyu Aziza ndiye ambaye alinifanya niwaone wasichana wote kuwa wa kawaida sana,
yeye ndiye aliyenifanya nimuone kuwa msichana mzuri kuliko wasichana wote
duniani. Uwepo wake katika mtandao wa facebook bado nilikuwa nauhitaji sana,
nilikuwa nikijisikia mpweke kupita kawaida. Aziza...Aziza...Aziza...upo wapi
wewe msichana uje kuupoza moyo wangu ulio kwenye maumivu makali?
Siku
zikaendelea kukatika na hatimae siku ambayo ilionekana kunifurahisha ikawadia.
Siku hiyo nikawa kama nimepigwa na mshtuko mkubwa moyoni, sikuamini kile
ambacho kilikuwa kikionekana machoni mwangu, Aziza alikuwa hewani. Sikutaka
kupoteza muda, sikutaka kuleta pozi, kwa haraka sana nikamtumia meseji.
MIMI:
Mungu wangu!
AZIZA:
Nini tena.
MIMI:
Umekuja at last.
AZIZA:
Yeah! Nilipotea kwa kipindi fulani hivi, si unajua mitihani wangu.
MIMI: Pole
sana. Mmekwishamaliza?
AZIZA:
Yeah! Tumekwishamaliza. Ila nami nilikumisi sana.
MIMI:
Nashukuru kwa kunimis, ila ulimiss nini kutoka kwangu?
AZIZA:
Chatting zako, meseji zako zimekaa kitofauti sana na watu wengine.
MIMI:
Kivipi?
AZIZA:
Zipo kitofauti sana. Katika maisha yangu nimewahi kuchati na watu wengi sana,
ila zako...dah!
MIMI: Bado
haujaniambia kivipi.
AZIZA: Kwanza
hauandiki kimkato kama neno ‘sijui kuliandika cjui’, yaani maneno ya mikato
huwa hauitumii kabisa.
MIMI:
Kwani hiyo nayo ni sababu?
AZIZA: Ngoja
nikwambie kitu Ibra. Hii ni siri ambayo wanaume wengi wamekuwa hawaielewi na
ndipo wanapofanya makosa kila siku.
MIMI: Siri
gani?
AZIZA:
Unajua unapochati na msichana yeyote ambaye haujawahi kuonana nae, unatakiwa
kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, hiyo ndio sifa moja kubwa ya kumteka msichana
kwa sababu hisia zetu hazitekwi na mambo makubwaaa, hapana, hivi vitu vidogo
vidogo ambavyo wavulana wanavipuuzia ndio vinatuteka.
MIMI: Kama
vitu gani.
AZIZA: Cha
kwanza salamu Ibra. Hivi unajua kwa sababu gani meseji yako ya kwanza kabisa
uliyowahi kunitumia sijakujibu?
MIMI:
Hapana. Sijajua kwa nini.
AZIZA:
Salamu. Wanawake wengi wanalichukulia tofauti neno ‘mambo’. Unapomsalimia
msichana kwa mara ya kwanza kwa kumwambia ‘Mambo’, wanaojibu ni wachache sana.
MIMI: Kwa
nini sasa?
AZIZA: Kwa
sababu mwanamke anapenda kufuatwa kinidhamu.
MIMI: Sasa
nilitakiwa kukusalimia vipi ili ujibu?
AZIZA:
Unapomfuata msichana yeyote duniani, anza kwa kumsalimia ‘Habari yako’ au
salamu yoyote iliyokaa kinidhamu. Kidogo ukisalimia hivyo, kuna asilimia kubwa
sana ya msichana kukujibu.
MIMI: Duh!
Kumbeee!
AZIZA:
Yeah! Hiyo ni siri ya kwanza Ibra, wavulana wengi huwa wanafeli hapo tu kitu
ambacho kinawafanya kila siku kulalamika kwamba wasichana tuna mapozi kujibu
salamu zao, hapana, hatuna mapozi bali wanakosea kusalimia, wanakosa nidhamu
katika kusalimia.
MIMI:
Nimekuelewa. Naomba siri nyingine.
AZIZA:
Chatting. Unajua usipende kuchati na msichana kifupi kama nilivyokueleza toka
mwanzo. Andika neno lote kwa ujumla, unajua unapoandika kifupi, unaupa kazi
ubongo wa mtu kulifikiria neno na matokeo yake akili yake inachoka na kukatisha
chatting na wewe.
MIMI: Ila
mimi sijawahi kuchati namna hiyo Aziza.
AZIZA: Najua.
Ila ninakumegea siri juu ya vitu ambavyo msichana anavipenda na vile
asivyovipenda.
MIMI: Dah!
Umeifungua akili yangu.
AZIZA: Ila
wewe..dah! Wewe mtu noma.
MIMI: Kwa
nini?
ITAENDELEA SIKU YA KESHO
Unataka niwe nakutumia CHOMEZO watu 200 wa
kwanza kulike PAGE YA 2JIACHIE Mtatumiwa imbox chomezo LIKE PAGE YETU
HAPA ==>www.facebook.com/2jiachie
Post a Comment