ad

ad

WANAOVAA MLEGEZO MARUFUKU SIMBA

KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amewakemea wachezaji wake wenye tabia ya kuvaa kaptura zao kwa kuanzia katikati ya makalio ‘mlegezo’ badala ya kuanzia kiunoni.
 Logarusic amefikia hatua hiyo kutokana na wachezaji hao kushindwa kutekeleza maagizo yake anayowaagiza wanapokuwa uwanjani, badala yake hutumia muda mwingi kushusha na kupandisha kaptura zao.

Logarusic akiwaambia mashabiki wa Simba katika mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam kuwa amewapiga marufuku wachezaji wake kuvaa mlegezo.

“Nimewambia wasivae mlegezo uwanjani kwa sababu wanashindwa kufanya kama ninavyowaagiza wafanye kwa faida ya timu.

“Lakini wao wamekuwa wakifanya kinyume na matakwa ya benchi la ufundi na badala yake muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa kupandisha na kuzishusha kaptura zao, jambo ambalo linawafanya wapoteze umakini uwanjani,” alisema Logarusic.

Hata hivyo, mashabiki hao walipomuuliza ni wachezaji gani ambao wamekuwa wakivaa mlegezo uwanjani, hakuwa tayari kuwajibu na badala yake aliwaambia: “Mtajionea wenyewe.”
Simba ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya Yanga, Mbeya City na Azam ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 40.
Powered by Blogger.