ad

ad

Rage: Mpira Pesa jiandaeni kwa virungu

MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage amejibu mapigo ya wanachama wa klabu hiyo, Tawi la Mpira Pesa waliotangaza kuandamana mpaka kwake, ambapo amewakaribisha kwa mikono miwili, lakini akisema kuwa waje wamejiandaa kukumbana na virungu vya Jeshi la Polisi.
Wanachama hao walitoa kauli hiyo juzi baada ya Yanga kumsajili aliyekuwa straika wa Simba, Emmanuel Okwi, ambapo walisema hawana imani na mwenyekiti wao, huku wakisema kuwa baada ya mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Yanga, kwa matokeo yoyote, lazima wataweka ‘kambi’ kwa Rage mpaka ajiuzulu uenyekiti.

Akizungumza katika mkutano na baadhi ya wanachama juzi makao makuu ya timu hiyo, Msimbazi, Kariakoo jijini, Rage alisema: “Naona hawajaridhika walivyokwenda bungeni, nasikia wanataka kuja kwangu, nawakaribisha, lakini wajiandae kwa virungu vya polisi wangu.“Nilipeleka taarifa hizo kwa polisi, kwa hiyo wakija wajue watakutana na dhoruba hilo.”
Powered by Blogger.