MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA BUMBULI ASIMAMISHWA UONGOZI
TAARIFA KWA UMMA
KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA JIMBO YA BUMBULI ABDI SHEKIMWAGA
KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA JIMBO YA BUMBULI ABDI SHEKIMWAGA
CHADEMA Kanda ya Kaskazini, inawatangazia
umma wote kuwa, Ndugu ABDI SHEKIMWAGA amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa
CHADEMA jimbo la Bumbuli kuanzia 21 Desemba 2013.
Ofisi ya kanda, ilipokea nakala ya taarifa
na miniti ya kikao kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka kamati
tendaji ya wilaya/jimbo pamoja na nakala ya barua ya tuhuma
alizoandikiwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA ili ajieleze na kujibu, ikiwemo na
barua ya tarehe 12 Desemba 2013 aliyoandikiwa katibu wa mkoa kujulishwa
mapendekezo na hatua za kunusuru chama dhidi ya hila mbaya zilizokuwa
zinafanywa na ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu SHEKIMWAGA
alitoa maneno ya kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa kwa
viongozi na kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo.
Uongozi wa Kanda baada ya kupitia taarifa
hizi na baada ya kufanya kikao cha pamoja na viongozi wa wilaya tarehe
21 Desemba 2013 huko wilaya lushoto mkoani Tanga, unamtangaza ndugu
SHEKIMWAGA kuwa kwa kukinisuru chama dhidi ya tuhuma dhidi yake, kwa
ajili ya kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya hofu na
kutokuwa na imani kulikoonyeshwa na viongozi na wanachama wenzake
AMESIMAMISHWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA KUANZIA TAREHE 21 DESEMBA 2013.
Hatua hii ni ya kuzingatia pendekezo la kamati tendaji ya wilaya/jimbo
kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (c), “amekoma kuwa kiongozi kwa kushindwa
kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni na maadili
ua chama”.
Aidha uongozi wa kanda, unaliagiza baraza
la uongozi la mkoa ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa wilaya/jmbo kwa
mujibu wa katiba ya chama ibara ya 6.3.6 (a) sehemu (iV) kuwa ndugu ABDI
SHEKIMWAGA APEWE FURSA NYINGINE TENA akiwa katika hali ya kusimamishwa
uongozi kwa kuandikiwa barua tena ya tuhuma dhidi yake na apewe muda wa
kikatiba kujibu ama sivyo hatua kali zichukuliwe dhidi yake.
Tuhuma hizo ni;
1. Kuamua kwa makusudi kuzuia na
kukwamisha kazi za CHAMA, programu ya CHADEMA ni msingi. Ndugu
SHEKIMWAGA ametoa maneno ya uzushi na upotoshaji kwa uwazi mbele ya
viongozi wenzake na maafisa wa kanda kuwa hayuko tayari kufanya kazi
ambayo yeyé aliitafsiri kuwa ina lengo la kumjengea mtu fulani mtandao
ndani ya chama. Hii ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na
uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1 (viii)
2. Ametoa lugha na matamshi yenye
kuonyesha udini na ukabila mbele ya viongozi wenzake na mbele ya maafisa
wa kanda kuwa kaimu katibu wa CHADEMA mkoa wa Tanga ndugu Jonathan
Leonard Baweje kuwa ni Mkristo na ametokea mkoa wa Kigoma hivyo hawezi
kuwa katibu wa mkoa wa Tanga kwa sababu sio muislam. Hii ni dhambi mbaya
sana na ni kinyume na kanuni ya maadili ya kiongozi na uendeshaji wa
kazi za chama sura ya 10.1 (iv), “Kiongozi yoyote asijihusishe na
vikundi vyovyote vyenye misingi ya ukabila, udini, au ukanda ambavyo
vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama au miongozi mwa jamii kisiasa
au kijamii”.
3. Amejitambulisha wazi mbele ya
viongozi wenzake na mbele ya maafisa wa kanda kuwa yeyé yupo kundi la
Zito Kabwe na atahakikisha CHADEMA inakufa Bumbuli iwapo maamuzi ya
kamati kuu ya kumvua uongozi Zito Kabwe hayatabadilishwa. Kitendo hiki
cha kujitengenezea makundi na upotoshaji ni kinyume na kanuni ya maadili
ya kiongozi na uendeshaji wa kazi za chama sura ya 10.1. (iv), “Ni
mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi halali ya vikao
vya chama”.
4. Amezuia kwa makusudi kazi za
chama na amekuwa akifanya hujuma dhidi ya viongozi wengine ambao
wamekuwa wakifanya kazi za chama. Sambamba na hili ametuhumiwa kuwa
anashirikiana na wapinzani wetu CCM katika kuhujumu chama na kwa kumwaga
sumu na maneno ya uongo. Kitendo hiki kimekuwa sababu ya kuzuka kwa
migogoro isiyokwisha katika jimbo la bumbuli na imeendelea kuvunja moyo
na kuleta mifarakano inayorudisha nyuma kazi za chama. Jambo hili ni
kinyume na kununi ya maadili ya uongozi na uendeshaji wa kazi za chama
sura ya 10.1 (ix), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au
vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au
wanachama wake”.
Taarifa hii inaenda sambamba na ndugu
ABDI SHEKIMWAGA kukabidhi vifaa vyote vya chama, ikiwemo kadi za chama
mpya zipatazo 400 zenye thamani ya Tshs 600,000 ndani ya siku TATU
kuanzia tarehe ya taarifa hii kwa KATIBU WA CHADEMA MKOA WA TANGA.
CHADEMA Kanda ya Kaskazini inaendelea
kuonya kuwa haitavulia kabisa kuona CHAMA CHETU ambacho ni tumaini kwa
Watanzania wengi kikivurugwa na watu wachache wenye hila mbaya na chafu.
Aidha nitoe rai kwa WanaCHADEMA wote wa kanda ya kaskazini na
Watanzania wapenda haki na kweli wasiwe na hofu yoyote na matukio haya
ya kukisafisha chama maana hatuna budi kusafisha na kufukuza bundi wote
waondoke.
Imetolewa leo tarehe 23 Desemba 2013
Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.
Makao Makuu ya Kanda – Arusha, Tanzania:
Simu: +255 754 912 914
Imetolewa leo tarehe 23 Desemba 2013
Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.
Makao Makuu ya Kanda – Arusha, Tanzania:
Simu: +255 754 912 914

Post a Comment