ad

ad

KOCHA WA SIMBA, TAMBWE NI KIBOKO

KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic,  amefurahishwa  na uwezo wa mshambuliaji wake, Amissi Tambwe na akasisitiza Mrundi huyo ni kiboko.
Tambwe alikuwa amemuudhi kocha huyo raia wa Croatia kutokana na kuchelewa kufika kambini, hali iliyosababisha uhusiano wa wawili hao kuyumba, lakini baada ya Mrundi huyo kuibeba Simba Taifa, Logarusic amechekelea na kusahau tofauti zao zote.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, Tambwe alitupia mabao mawili, moja likafungwa na Awadh Juma.

Akizungumza kocha huyo alisema katika mchezo huo, safu ya ushambuliaji iliweza kumtendea haki.
 “Safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Tambwe ilikuwa nzuri, yenye uwezo na kiwango kinachovutia,” alisema Logarusic.

Powered by Blogger.