ad

ad

Brandts awataja walioiua Yanga SC


KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts,  amewataja waliochangia kuimaliza Yanga dhidi ya wapinzani wao Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi.

Yanga ilishindwa kutamba juzi mbele ya Simba baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Akizungumza  Brandts alisema kosa alilolifanya kipa Juma Kaseja la kufanya mbwembwe karibu na lango, kisha kusababisha bao la tatu, lilichangia timu hiyo kufanya vibaya.

Ukiachana na hilo, Brandts alisema wachezaji wake katika mchezo ule, walicheza kama siyo wa timu moja, kitu ambacho kilichangia kufanya vibaya.

“Wachezaji hawakucheza kama timu na maprofesheno ninao wengi katika kikosi changu lakini walishindwa kuonyesha uwezo wao katika mchezo, japo kipa naye alifanya kosa ambalo lilisababisha kuwapa nafasi Simba kupata bao rahisi sana.
“Japo hata mfumo tuliotumia nao ulisumbua kidogo ila wachezaji wanapaswa kutambua nini wanachofanya wanapokuwa uwanjani, ingawa kipindi cha pili walijitahidi,” alisema Brandts.
Powered by Blogger.