Shetta na Diamond Platinum waingia Studio kutengeneza wimbo mpya wa kufungia Mwaka 'Mama Qayllah'
Ukianza kutaja nyimbo zilizofanya vizuri mwaka 2012 basi lazima
utaje wimbo unaofahamika kwa jina la 'Nidanganye Nidanganye' uliyoimbwa
na Shetta aliyomshirikisha Naseeb Abdul aka Diamond Platium
Sasa habari njema nyingine kutoka kwa Shetta akizungumza na tovuti ya
100.5 leo Novemba 28 amesema kwasasa yupo katika hatua ya maandalizi ya
wimbo wake mpya 'Mama Qayllah' aliyomshirikisha Diamond Platinum,wimbo
umetengeneza Burn Records chini ya producer 'Sheddy Clever'
'Shetta hapa ama niite Baba Qayllah,kwanza kabla ya yote ningependa
kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya
wimbo wangu 'Sina Imani',kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu
mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo
unaitwa Mama Qayllah bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing
na Sheddy Clever wa Burn Records,Kwa hiyo wewe shabiki kaa tayari hapa
Baba Qayllah pale Platinum ebu Angalia Mbele'Alisema Shetta.
Katika mazungumzo Shetta alidai kuwa huu ndio utakuwa ni wimbo wake wa kufungia Mwaka 2013.
CREDIT: TIMES FM

Post a Comment