ad

ad

SHARO MILIONEA ATIMIZA MWAKA TANGU ALIPOFARIKI

 Marehemu Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’( 1985 - 2012 ) enzi za uhai wake.
Hili ndio Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Marehemu Sharo Milionea alifariki dunia tarehe 26 Novemba , 2012 kwa ajali mbaya ya Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR wakati akitoa Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga.Alipofika maeneo ya maguzoni nje kidogo na wilayani Muheza gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali.
Powered by Blogger.