JUMUIYA YA WANA-MASOKO YA WANAFUNZI WA CBE WAANDAA MHADHARA WA WAZI
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)wakimsikiliza
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(hayupo pichani) ambae
ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa kwenye mhadhara wa wazi
ulioandaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuoni hapo.
Naibu
Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dr. Abby Nangawe akiongea muda
mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa wazi ulioandaliwa na Jumuiya ya
Wana-masoko ya wanafunzi wa chuo hicho.Katika ni Mkuu wa Idara ya Masoko
wa Vodacom Kelvin Twissa ambae ndie aliyekuwa mzungumzaji Mkuu mwalikwa
kwenye mhadhara huo na kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE
Godian Bwemelo.Mhadhara huo ulifanyika jana chuoni hapo jijini Dra es
salaam.
Mkuu
wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akizungumza na Jumuiya ya
wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA)
chuoni hapo jana. Twissa alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo wa wazi
chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta ya masoko na
wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobebea
katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo vyuoni
kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
Mkuu
wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Tiwssa akionesha kwa vitendo mbinu
za kimasoko Wakati alipoalikwa kuzungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya
wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana.
Twissa ni mmoja kati ya vijana waliobobea katika Nyanja ya masoko na
matangazo nchini na alialikwa chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake
katika sekta hizo na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia
wafanyakazi wake waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika
midahalo ya aina hiyo vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
Post a Comment