Happiness Watimanywa ndiye Redd’s Miss Tanzania 2013.
MREMBO Happiness Watimanywa kutoka Dodoma Kanda ya Kati, juzi
usiku kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam alitawazwa
kuwa Redd’s Miss Tanzania 2013 baada ya kuwabwaga wenzake 29.
Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara
baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni
mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo
Warembo hao, walianza kwa shoo ya vazi la ufukweni kisha la jioni.
Happiness ambaye pia ni Miss Photogenic, alionyesha uwezo mkubwa katika kipengele cha maswali na kuuteka ukumbi mzima.
Mshindi wa pili aliibuka Latifa Mohamed wa Kanda ya Temeke, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Clara Bayo pia wa Temeke.
Kwa ushindi huo, Happiness alizawadiwa gari na kitita cha sh milioni 8.
Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa kundi la Mama Afrika,
Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ambaye aliwabamba vilivyo mashabiki huku
msanii kutoka Uganda, Mike Ross, akishindwa kukonga nyoyo za
waliohudhuria.
![]() |
| Hawa ni warembo walioingia hatua ya tano bora. |
Hawa ni warembo walioingia hatua ya 15 bora.



Post a Comment