Sporah Njau kuwakilisha 'bongo movies' kwenye tuzo za filamu za ZAFAA 2013.
Hivi karibuni muandaaji wa kipindi maarufu cha The
Sporah Show, Sporah Njau aishiye nchini Uingereza alichaguliwa kuwa
mwakilishi wa Afrika Mashariki kwenye tuzo kubwa barani Afrika, ZAFAA
Awards 2013.
Tovuti ya Bongo5 ilifanya naye mahojiano ili kujua zaidi
majukumu yake kwenye tuzo hizo. Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo.
Unadhani kwanini ulichaguliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki?
Unadhani kwanini ulichaguliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki?
Naamini sababu kubwa kabisa ni kwamba mimi mwenyewe ni mzaliwa
wakutoka Afrika Mashariki.
Pili ni kwamba, nimekuwa kwenye TV screen za
watu hapa Uingereza na Europe kwa ujumla kwa muda wa miaka zaidi ya 5,
na kwajuhudi zangu zaidi nimebarikiwa kuwa mmoja wa wanawake wenye
ushawishi mkubwa hapa Uingereza. I have amassed a great fortune through
my media interests and use my TV Show to positively influence of the
young generation.
Ukiwa kama mwakilishi, kazi yako ni ipi hasa?
Kazi yangu ni kuwataarifu wana filamu wa Afrika Mashariki kuhusu
fursa hii ya pekee ambayo ni fursa ya wao kuitangaza nchi na kutangaza
filamu zao katika ngazi za juu. Na pia kualika viongozi wa serikali wa
nchi hizo na balozi ili kushuhudia tunzo hizo zitakazofayika kwa siku
tatu hapa nchini Uingereza.
Muitikio wa wasanii wa nchi za Afrika Mashariki kutuma kazi zao ukoje?
Kusema ukweli muitikio sio mbaya, nchi za Afrika Mashariki
zimejitokeza na kutuma kazi zao. Fingers cross filamu zao zifanikiwe
kufikia vigezo vyote vinavyihitajika katika ZAFAA AWARDS 2013. (The
Quality of the Movie eg: Picture & Sound)
Umepokea filamu za kutosha kutoka Tanzania?
Sijui hata nianzie wapi kujibu hili swali maana ni aibu kwangu
mimi. Mpaka sasa ZAFAA AWARDS 2013 haijapokea filamu yoyote kutoka nchi
yaTanzania, ila bado sijafa moyo, hivyo bado nasubiri, nimekua nikisema
labda kesho, labda kesho lakini naona siku zinazidi tu kusonga.
Hopefully tutapata hata moja maana ninavyojisifiaga kwa watu na movie
zetu za Bongo.!! hahaha..!
Nigeomba watunzi wa filamu za Tanzania wasiniangushe kwakweli.
Waandaaji na hata waigizaji wajitokeze kuchukua fursa hii, na kutuma
filamuzao. Hata kama hawatashinda au hawatafanikiwa kufikia kile kiwango
ambacho kinahitajika katika ZAFAA AWARDS 2013.Uzuri wa ZAFAA AWARDS ni
kwamba filamu yako kama haitafanikiwa kuingia katika mashindano, basi
watakupa sababu za kwanini filamu hiyo haijafanikiwa kufikia kile
kiwango chao ZAFAA AWARD.Which I believe Positive or negative feedback
is a gift because you can learn from that, ili wakirecord filamu
nyingine wataziweke kwenye standard ambayo inakubalika kimataifa.
Ni vigezo gani vinavyotumika kuja kupata filamu bora?
Kigezo kikubwa ni picture quality and sound, then the Story, na je hiyo
filamu ilifanya vizuri kiasi gani locally (Original Country).
Kigezo kikubwa ni picture quality and sound, then the Story, na je hiyo
filamu ilifanya vizuri kiasi gani locally (Original Country).
Filamu zinazohitajika ni za Kiingereza tu ama hata lugha nyingine pia?
Hapana, Filamu zinazohitajika sio lazima ziwe kwa Lugha ya
Kiingereza. Lugha yoyote inakubalika ili mradi tu iwe na Subtitles ya
kiingereza.
Mwisho unatoa ushauri upi kwa waigizaji wa Tanzania utakowasaidia kupata mafanikio kimataifa kuliko ilivyo sasa?
Kwanza kabisa, ni ku jump into any kind of opportunity ambayo
itakusaidia kuipa career yako exposure, maana hatujui lini au wapi
mafanikio yatajitokeza. Wakati mwingine Grabbing opportunities can seem
scary but we’ll never know if we don’t go for it; I hate to think of the
woulda,coulda, shoulda’s.
Also, Self Marketing as an artist is crucial to your success, as
a movie star, a director or a producer, I think it is important to take
all the opportunities that comes way, and thriving on the chances – and
whatever happens next. Mungu ndiye anaejua, angalau unasema nilijaribu,
kuliko “I WISH” (Laiti ningelijua)
Kuna msemo wa mtu maarufu anaejulikana kama Milton Berle unaosema “If opportunity doesn’t knock, build a door”
Watanzania tunatakiwa kujua kwamba opportunity is not a lengthy visitor,
means that we need to learn to take advantage of an opportunity before
it disappears;, Good things don’t wait around forever.
Post a Comment