Wanaume wanavyoibiwa kwa ‘I love U, I miss U baby!’.
Unaweza
kukutana na msichana mzuri sana, ukampenda na kudhani anaweza kuwa
mkeo. Yeye akishabaini umemzimikia, anakuwekea mapozi ya kimtindo kwa
muda kisha anakukubalia.
Kwa kuwa na wewe umeoza kwake, utakuwa
tayari kumfanyia chochote ili uweze kumshikilia. Akilini mwako unajipa
matumaini kuwa uko peke yako na huyo atakuwa mkeo siku zijazo kumbe
mwenzako ana lengo la kukuchuna tu.
Atatumia maneno matamu
kukulainisha lakini mizinga itakuwa sehemu ya maisha yake. Kwa kuwa na
wewe unampenda na hauko tayari kumkosa, utakuwa ukimpa pesa na huduma
nyingine.
Unajua kitakachotokea? Huenda hujui lakini wengi wanafanya hivi; anakupiga mizinga sana hadi inafikia hatua unamchukia na kuhisi hakufai.
Unajua kitakachotokea? Huenda hujui lakini wengi wanafanya hivi; anakupiga mizinga sana hadi inafikia hatua unamchukia na kuhisi hakufai.
Kuhisi kwako hakufai ndiyo furaha kwake kwani na yeye
hakuweka akilini mwake kuwa anataka kuolewa na wewe. Matokeoa yake
unabaki ukiumia kumkosa na pia itakuuma zaidi kwa kuwa ametumia pesa
zako nyingi bila kufanikisha kile ulichodhamiria.
Hivyo ndivyo ilivyo
sasa na kwa mfano kuna hii mitandao ya kijamii kama vile Facebook. Huku
wanaume wengi wanalizwa na hawa mabinti wajanja wa mjini.
Msichana
anaweza kukuomba urafiki ukamkubalia, baada ya muda anajitongozesha
kwako kwa kudai amekuzimikia. Kama na wewe utakuwa limbukeni na ukadata
na mtu ambaye wala humjui lakini maneno yake yakakuvutia, tarajia
kulizwa.
Nasema hivyo kwa kuwa, ni lazima ataonesha kukupenda sana na
atakuwa akikuandikia maneno matamu kama vile I love you, I miss you na
mengineyo ya aina hiyo na ukishakolea si ajabu akaanza kukuambia anataka
kuonana na wewe ila kwa kuwa yuko mbali anataka umtumie nauli.
Lakini
hata kabla ya kukuambia umtumie nauli, anaweza kuwa ameshakuomba pesa
nyingi, vocha za kutosha na wewe ukawa unamtumia ili kulilinda penzi
lenu.
Sasa mwisho wa mawasiliano yenu utakuwa pale ambapo atakuomba umtumie nauli ili aje muonane, ukishamtumia tu anaingia mitini na huwezi kuamini msichana huyo anaweza kuwa na wanaume wengi anaowafanyia hivyo.

Wengine
hawatumii mtandao wa Facebook bali hutumia simu zao kuwaingiza mjini
wanaume. Kwa kifupi huo ni mchezo ambao upo na wanaume wengi
wameshalizwa.
Kikubwa ni watu kuwa makini na hawa wasichana warembo wanaojirahisi kwa wanaume. I love you, I miss you ni maneno tu ambayo anayeyatamka anaweza akawa hamaanishi hivyo bali anataka kukupumbaza tu na ukiingia kwenye laini akuchune weee mpaka mwenyewe uachie ngazi kisha yeye anahamia kwa mwingine.
Ni hayo tu kwa leo.

Post a Comment