ad

ad

Vurugu za Mtwara: Bunge laahirishwa, laitaka serikali kutoa taarifa kesho.

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango akichangia hoja bungeni leo
Mtwara, 
Kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi ya leo yalitawala na huduma zote za kijamii zilifufungwa,usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kilichoendelea Mtwara ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake.
 Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. 
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi)  
 Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni
Powered by Blogger.