Papa ameagiza uchunguzi wa haraka mlipuko wa bomu Arusha.
OFISI ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis Jorge Mario imepokea taarifa za Kanisa Katoliki Parokia ya Ollasiti kulipuliwa na bomu nchini Tanznaia na kuiagiza serikali kutoa taarifa za uchunguzi wa suala hilo haraka.
Taarifa zilizonaswa vyanzo vya
kuaminika ndani ya kanisa hilo jijini Dar es Salaam zinadai kwamba Papa
Mario ameagiza serikali kutoa taarifa za uchunguzi wa suala hilo
haraka.
Papa Mario amepokea taarifa hizo ambazo zilitangazwa na Rais Jakaya
Kikwete kwamba ni tukio la kigaidi, huku watu watatu wakiuawa na wengine
zaidi ya 70 kujeruhiwa katika tukio hilo.
Akizungumza na Redio Vatican pamoja na mitandao ya kijamii inayomilikiwa na Kanisa hilo kubwa Duniani, mwakilishi wa Papa huyo Francisco
Montecillo Padilla alisema kwamba tukio hilo halikutarajiwa kabisa kwa
sababu muda wote kulikuwa na hali ya utulivu na amani kanisani hapo.
"Nilipata mshtuko baada ya kusikia mlipuko wa bomu hilo, na
sekunde chache nikaona majeruhi wengi wamelala chini, nikapatwa na wasi
wasi huku nikiwaonea huruma majeruhi wasiokuwa na hatia lakini Askari
Polisi waliwahi kunichukuwa na kunipeleka sehemu iliyotulia kwa usalama
zaidi"alisema Askofu Montecillo Padilla.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kwamba Ofisi ya Papa Francis
tayari imeiagiza Serikali ya Tanzania kuhakikisha inakamilisha uchunguzi
wa suala hilo haraka, huku pia ikionyesha nia ya kutoa msaada zaidi kwa
serikali katika uchunguzi wake. Hata hivyo Ofisi ya
Kiongozi huyo tayari imesha agiza Kikosi cha upelelezi cha kimataifa
kutoka nchini Marekani FBI kuja nchini kuongeza nguvu katika upelelezi
wa tukio hilo,tukio la aina hiyo halikuwahi kutokea nchini Tanzania, ila
liliwahi kutokea katika nchi jirani ya Kenya.
Habari imeandaliwa na Belinda Masangula na Editruda Mashimi kwa msaada wa mashirika ya habari
Post a Comment