Necta wagoma kufuta matokeo IV,watishia kujiuzuru.
Dar es Salaam,Tanzania
WAKATI Serikali ikitangaza kufuta matokeo ya mtihani wa kidato
cha nne, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni
Makamu Mkuuwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Mukandala
amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Necta Joyce Ndalichako
Chanzo
cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa
taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.
Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.
Habari za kuaminika zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philipo Mulugo
alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo iliita
bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi akisema, "Sorry I'm
busy call back later", alisema Mulugo kupitia simu yake ya mkononi.
Post a Comment