Mke amzuia Niyonzima kusajili Simba.
MKE wa kiungo wa Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas'
anayeitwa, Naillah Uwineza amemwambia mumewe furaha yake ni kumuona
akicheza Ulaya msimu ujao lakini kama itashindikana basi abaki Yanga.
Mke wa Niyonzima, Naillah Uwineza.
Niyonzima amemaliza mkataba wake na Yanga na amefanya mazungumzo na Simba na Yanga na hata Azam imetajwa kuanza kumnyemelea kwa taratibu.
Niyonzima amemaliza mkataba wake na Yanga na amefanya mazungumzo na Simba na Yanga na hata Azam imetajwa kuanza kumnyemelea kwa taratibu.
"Kama ni amri yangu napenda mume wangu (Niyonzima) aende kucheza Ulaya. Kama unavyojua Ulaya ni Ulaya tu tofauti na mazingira ya hapa kwetu Afrika, kule kuna mafanikio zaidi,"alisema Naillah.
Haruna Niyonzima
"Lakini, kama itashindikana basi wasikilizane na mabosi wake tu abaki Yanga. Hapa Yanga ndiyo alipo na amezoeleka kwa sababu amecheza kwa muda mrefu. Pia naona ndiyo timu kubwa na yenye mafanikio kwa sasa, naona abaki Yanga tu,"alisisitiza Naillah ambaye pia ni Mnyarwanda lakini anaishi Dar es Salaam na mumewe.

Usajili wa Niyonzima umekuwa ukitikisa jiji la Dar es Salaam kutokana na kiwango chake uwanjani hali iliyosababisha klabu mbalimbali kumtolea macho.
Niyonzima alisajiliwa na Yanga miaka miwili
iliyopita akitokea APR ya Rwanda na kwa muda mrefu amekuwa katika
kiwango kikubwa cha soka.

Post a Comment