Madrid yathibitisha kuachana na Mourinho
Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ataondoka kwenye kibarua cha kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Rais wa klabu ya Real Madrid,Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari jumatatu jioni kuwa Mourinho hatofukuzwa bali wamekubaliana kumaliza mkataba wao na kocha huyo raia wa Ureno.
Aidha Madrid, imeongeza kuwa haijaanza
mazungumzo na kocha yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi ya Mourinho
lakini vyanzo mbalimbali vya habari za michezo zinamtaja kocha wa PSG ya
Ufaransa, Carlo Ancelloti kuchukua jukumu la kuifundisha Madrid msimu
ujao.
Duru za kimichezo zinasema, Jose Mourinho huenda
akarejea nchini Uingereza kuifundisha klabu yake ya zamani ya Chelsea
baada ya kuwepo makubaliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo.

Post a Comment