KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI.
KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na
simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata
akina mama wengi wakati wa hedhi nimeona ni bora niandike makala hii ili
iweze kuwasaidia na wengine kujua nini chanzo na mhusika afanye nini
pale anapopatwa na tatizo hilo.
Maumivu wakati wa hedhi
(period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza
sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata
siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya
wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu
hayo huanza pale yai linapotoka katika mrija (fallopian tube) na
kuteremka chini ya mrija huo wakati wa Ovulation.
AINA YA MAUMIVU
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili. Ya kwanza ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili ni yale
maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za
kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na
matatizo katika mirija ya mayai.
Nusu ya wasichana na wanawake hupata
maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kumi mpaka kumi na tano
wanasema kuwa hupata maumivu makali.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
Uchunguzi unaonesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
Sababu
hizo ni kama kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo wakati wa
miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutoka damu nyingi wakati wa hedhi,
wanawake ambao hawajawahi kuzaa.
Magonjwa yanayoweza kusababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:
Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuoka nje ya fuko hilo, au hata sehemu nyinginezo
Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.

PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga.
Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.
Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

Post a Comment