TIMBWILI : MUME wa mtu nusura auawe na KIMADA
WAKATI
Oparesheni Fichua Maovu katika jamii inayoendeshwa na Global Publishers
ikiwa kazini, wikiendi iliyopita ilinasa timbwili ‘hevi’ la aina yake
kwa mwaka 2013 ambapo mume wa mtu, Joseph Hussein (31), nusura auawe na
kimada, Ijumaa Wikienda linakumegea sinema ya bure. Tukio
hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge, Dar mishale ya saa
10 usiku ambapo mwanaume huyo, mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo
almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina
Neema Samson, mkazi wa Buguruni.Habari
za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni mume wa
mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi lakini
akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama wanavyokubaliana.
Fichua
Maovu ikiwa mzigoni kunasa matukio machafu katika jamii likiwemo lile
sugu la usaliti kwa wanandoa, ilipofika eneo la tukio, ilisikika sauti
ikitokea gizani ikiita, mwizi…mwizi…mwizi…Timu
ya Ijumaa Wikienda ilitii sauti hiyo na kuelekea kule ilikokuwa
ikitokea ambapo Neema alikuwa amemkwida shingoni Joseph huku akilalamika
kuwa anataka ujira wake.
SEKESEKE LAFUNGA MTAA
Kutokana
na sekeseke hilo la kupigana, watu kibao walitoka nje ya nyumba zao na
kushuhudia kilichotokea ambapo walipigwa na butwaa huku wakilalamika
kuwa waliamshwa usingizini na watu waliokuwa kwenye starehe zao.
WAAMKA NA BOKSA, NIGHTDRESS
Huku
wakiwa na boksa, night dress, vipensi na wengine mataulo, majirani wa
eneo hilo walimshuhudia Neema akiwa amemkaba Joseph shingoni hadi
akashindwa kupumua na kusababisha hekaheka mtaa mzima.“Kha! Mwanamke amemkaba mwanaume anataka kumuua kisa ni nini?” alihoji mmoja wa majirani hao.
Neema alikuwa akimnyonga Joseph kwa kutumia fulana yake akilalama kuwa
amezoea kupewa penzi kisha kuingia mitini bila kulipa.“Namjua ni mume wa
mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama hamuamini niwaoneshe (huku
akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka buku kumi na tano yangu la
sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa hasira.Wakiwa eneo la
tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia wakigaragazana
mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu yake aina ya
Nokia.
MJUMBE ATEMA CHECHE
Kwa upande
wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote kuwaamua
lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph akidai ujira
wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti, alikuwa
ameshanyang’anywa na wasamaria wema.
SOO HILOOO POLISI
SOO HILOOO POLISI
Wawili hao
waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema waliposhirikiana kuwabeba kisha
kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo cha polisi....
Picha zaidi za tukio angalia hapa chini
Habari na Global Publishers
Post a Comment