Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa
Kilosa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye amesema Chadema ni chama kilichovamiwa na watu wanaotumia siasa kuganga njaa.Nape alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye
“Ndugu zangu kuweni macho kwa sasa, siasa imeingiliwa na watu wasiokuwa na sifa za uongozi na kazi yao kubwa ni kutumia siasa kuganga njaa zao,” alisema.
Alisema wananchi wanapaswa kuwa macho na wanasiasa hao ambao malengo yao ni kuwaangamiza wananchi.

Akitaja baadhi ya sifa za wanasiasa aliowaita makanjanja, Nape alisema wengi wao ndiyo wanaotaka madaraka kwa gharama yoyote.
“Moja ya sifa kubwa ya wanasiasa hawa ni pamoja na kutaka madaraka kwa gharama zozote hata ikiwa ni pamoja na kuondoa uhai wa mtu,” alisema.
Alisema Chadema wanachojua kwa sasa ni
kuwahujumu wale wote wenye mawazo tofauti na yao kwa kuwatesa na hata
kupoteza maisha ya wanaowapinga.
“Badala ya kushindana kwa hoja na sera, wanachokijua wao ni kung’oa kucha za wanaowapinga, kuwatesa na wakati mwingine hata kumwaga damu kwenye operesheni zao,” alisema.
“Badala ya kushindana kwa hoja na sera, wanachokijua wao ni kung’oa kucha za wanaowapinga, kuwatesa na wakati mwingine hata kumwaga damu kwenye operesheni zao,” alisema.
Alisema kwa kuwa wamekusudia kwa gharama yoyote kushika dola, hawajali damu za Watanzania zinazomwagika ili mradi wanafanikisha wanalolitaka.Akikumbushia operesheni mbalimbali zilizofanywa na Chadema nchini tangu uchaguzi uishe mwaka 2010, Nape alitoa mifano ya operesheni ya mjini Arusha, Morogoro, Iringa, Singida na kwingine ambako maisha ya baadhi ya Watanzania yalipotea lakini hawakushtuka wala kuwajibika.
“Tunamwamini Mungu hataruhusu damu hizi ziendelee kumwagika kisa wanasiasa makanjanja, pia laana ya damu hizi zilizomwagika zitaviua vyama hivi na nchi yetu itabaki salama,” alisema.
Nape alitoa wito kwa wananchi kuwa macho dhidi ya wanasiasa wa namna hiyo.
“Hewa wanayovuta wanasiasa makanjanja ni ya watu wanaowaunga mkono, tunaweza kuamua leo kuwanyima hewa hiyo na huo ndiyo utakuwa mwisho wao,”alisema Nape.
“Hewa wanayovuta wanasiasa makanjanja ni ya watu wanaowaunga mkono, tunaweza kuamua leo kuwanyima hewa hiyo na huo ndiyo utakuwa mwisho wao,”alisema Nape.
Post a Comment