Abdul apewa namba ya Twite
BENCHI la Ufundi la Yanga limethibitisha kuwa beki Juma Abdul ndiye atakayecheza nafasi ya Mbuyu Twite.
Yanga ambayo inasaka pointi 10 kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu huu huku ikiwa na mechi tano mkononi, leo Jumamosi itacheza na Oljoro JKT ya Arusha jijini Dar es Salaam.
Mtanange huo utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini Yanga itamkosa beki wake mahiri Mnyarwandwa Mbuyu Twite ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Lakini, benchi la ufundi limesema pengo la kiraka huyo litazibwa vema na mlinzi wa kulia Juma Abdul. Kocha msaidizi wa timu hiyo, Fred Felix Minziro alisema: Ni mchezaji muhimu kwetu lakini imeshatokea hawezi kucheza kwenye mchezo huo, hivyo hatuna budi kumtumia mchezaji mwingine kucheza nafasi hiyo.
Nafasi yake atacheza Abdul (Juma). Ni beki mzuri ambaye anajua majukumu yake. Tunaamini atacheza vizuri na kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri, alisema Minziro.
Pia, beki Juma Abdul alisema anaamini atacheza vizuri kulingana na maandaliizi ambayo wamefanya na anajua umuhimu wake kikosini.
Twite amengara na Yanga msimu huu kutokana na uwezo wake wa kucheza kama kiraka na kupachika mabao pamoja na kurusha mipira.

Post a Comment