Rais Jakaya Kikwete aifuata Azam Chamazi
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete,
anatarajiwa kuitembelea Klabu ya Azam, Championi Ijumaa limefahamishwa.
Mmoja wa mabosi wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina
lake litajwe, alisema Rais Kikwete anatarajiwa kutua katika Uwanja wa
Chamazi uliopo eneo la Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mapema
wiki ijayo.
Bosi huyo alisema mara baada ya kutua kwa Rais Kikwete
katika eneo hilo, atapata nafasi ya kuangalia maendeleo ya klabu pamoja
na kufungua uwanja mpya wa klabu hiyo unaojengwa kwa kasi pembeni ya
uwanja wa sasa.
“Uongozi upo katika maandalizi makubwa katika ugeni
huo mzito na kikubwa nadhani rais amevutiwa kirahisi kuja huku kutokana
na maendeleo ya haraka ambayo timu yetu imekuwa ikiyapata,” alisema bosi
huyo.
Naye Katibu Mkuu wa Azam, Nassoro Idrissa alikiri kuwepo kwa mpango wa ziara hiyo ya rais na kusema kila kitu kitakapokuwa sawa, uongozi wake utatangaza rasmi juu ya jambo hilo.
Naye Katibu Mkuu wa Azam, Nassoro Idrissa alikiri kuwepo kwa mpango wa ziara hiyo ya rais na kusema kila kitu kitakapokuwa sawa, uongozi wake utatangaza rasmi juu ya jambo hilo.

Post a Comment