MENEJA wa klabu ya Barcelona,Tito Vilanova anaweza kurejea katika benchi la ufundi wiki ijayo.
MENEJA
wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova anaweza kurejea katika benchi la
ufundi wiki ijayo wakati timu yake itakapochuana na Paris Saint Germain
katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
MENEJA
wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova
Mapema wiki hii Vilanova alirejea nchini Hispania badda ya kupatiwa
matibabu ya kansa kwa miezi miwili jijini New York, Marekani.
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 44 ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo
kutoka kwa Pep Guardiola mwanzoni mwa msimu huu alirejea katika mazoezi
ya klabu hiyo lakini alishauriwa kutosafiri na timu hiyo katika mchezo
wa leo wa La Liga dhidi ya Celta Vigo.
Kwa upande mwingine beki wa
kimataifa wa Ufaransa na Barcelona, Eric Abidal ametajwa katika kikosi
kitakachocheza na Celta Vigo baada ya kupita mwaka mmoja baada ya
kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini lingine.
Abidal mwenye umri wa
miaka 33 alifanyiwa upasuaji huo mwaka jana baada ya uvimbe
uliogundulika kwenye ini lake Machi 2011 kurejea tena.

Post a Comment