ad

ad

MANCHESTER UNITED 1 – REAL MADRID 2 …RONALDO ATOKA KICHWA CHINI, MOURINHO AKIRI MAPUNGUFU ASEMA TIMU BORA IMETOLEWA

Habari na Saluti5(www.saluti5.com)
RON IN A MILLION ... Rafael trying to get to grips with Real's star man
MANCHESTER UNITED imeyaaga mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupokea kipigo cha 2-1 kwenye uwanja wake nyumbani dhidi ya Real Madrid.
United ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya beki wa Real Madrid Sergio Ramos kujifunga dakika ya 48.
Mpira ulianzia kwa Van Persie upande wa kulia akuupiga mpira na kuokolewa kabla ya Luis Nani kuunasa na kumpelekea Danny Welbeck ambaye aliupiga na mpira ukamgonga Ramos na kwenda wavuni huku kipa Dieogo Lopez akiwa kapotezwa.
NAN ON A MISSION ... Nani has been given a chance to prove his worth
Luis Nani akiwafungisha tela mabeki wa Real Madrid
Kabla ya hapo Manchester United walinyimwa goli ambalo lilivuka mstari kabla haujaokolewa.
Dakika ya 57 mwamuzi Cuneyt Cakir akatoa maamuzi ya kushangaza baada ya kumpa kadi nyekundu ya utata Luis Nani kwa madai ya kumchezea rafu beki Arbeloa.
Luis Nani aliruka hewani kuufuata mpira wa juu kwa mguu, wakati anakwenda juu Arbeloa akawasili na kukutana na mguu wa Luis Nani wakati anashuka chini na wote wawili wakadondoka na kuugulia maumivu.
Lakini kwa mshangao wa wengi, Luis Nani alipoinuka akakutana na kadi nyekundu ya moja kwa moja kutoka kwa mwamuzi huyo raia wa Uturuki mwenye umri wa miaka 36 na kuanzia hapo mchezo ukabadilika.
HELPING HAND ... Jose Mourinho pats his fellow countryman on the back
Mourinho akimfariji Luis Nani baada ya kutolewa
Real Madrid waliokuwa wamefichwa kwa kiasi kikubwa wakaanza kusukuma mashambuli mbele na dakika ya 66 Modrick aliyetokea benchi akaisawazishia timu yake kwa shuti kali lililogonga nguzo na kujaa wavuni.
Dakika tatu baadae Cristiano Ronaldo akaifungia Real Madrid bao la pili na kukataa kushangilia.
LUKA ME NOW ... Modric shows Spurs fans what they're missing
Modric akifumua shuti lililozaa goli la kwanza
RON SEALS IT? ... Ronaldo's goal looked to have sent United out of the competition
Ronaldo akinyanyua mikono kupinga kushangilia goli lake
Dakika kumi za mwisho mpira uliweka kambi ya kudumu kwenye lango la Real Madrid lakini kipa Lopez alikuwa mwiba kwa United kwa kufuta michomo mingi.
GETTING TO GRIPS WITH THE OPPOSITION ... Sergio Ramos grabs Danny Welbeck's shirt
Mambo yalipokuwa magumu kwa Ramos
Baada ya mpira kumalizika Ronaldo aliyeichezea United kabla ya kujiunga Madrid alitoka kichwa chini na kukwepa shamra shamra za wachezaji wenzake huku mara chache akiinua macho yake yaliyoonyesha simanzi kwa mashabiki wa United na kuwapungia.
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho alipohojiwa kuhusu utata wa mwamuzi, aliongea maneno machache na kuondoka: “Mbali na mwamuzi, timu bora imetolewa, hatukucheza vizuri, hatukustahili kushinda”.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Hispania timu hizo zilifungana 1-1.
MAN UNITED: De Gea, Rafael, Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Cleverley, Nani, Welbeck, Giggs, Van Persie. Subs: Rooney (Cleverly 73), Young (Welbeck 80), Valencia (Rafael 87).
REAL MADRID: Diego Lopez, Arbeloa, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain. Pepe (Ozil 71), Kaka (Di Maria 45), Modric.
Powered by Blogger.