JUSTIN BIEBER AKERA MASHABIKI WAKE AZOMEWA JUKWAANI
LONDON, ENGLAND
SUPASTAA
mtoto wa muziki wa pop, Justin Bieber amezomewa na mashabiki ‘watoto
wenzake’ na wazazi wao baada ya kuchelewa kuanza shoo kwa saa mbili
ndani ya 02 Arena jijini London, Jumatatu usiku.
Mwimbaji
huyo Mcanada aliyesherehekea miaka 19 ya kuzaliwa Ijumaa iliyopita,
alitakiwa kuwa kwenye steji saa 2.30 usiku, lakini hakutokea hadi saa
4.20.
Mashabiki
wake wengi – ambao walikuwa watoto wa umri mdogo – wakati huo tayari
walikuwa wamerudishwa majumbani kwa ajili ya kuwahi kuamka kwenda shule
Jumanne asubuhi, huku wengine wakitokwa machozi kwa kutoona shoo yake
ambayo walilipa hadi pauni 331 kwa tiketi.
Wafuasi
wake kutoka Canada wanaojiita Beliebers ambao wamekuwa wakifuata shoo
zake maeneo mbalimbali, pia walikerwa na uchelewaji huo wa kipenzi chao.
Watu
20,000 tayari walijazana uwanjani saa 12.30 jioni — na wazazi wao
walirudi kuwachukua saa 4 usiku ambapo shoo hiyo ilipangwa kumalizika,
lakini wakati huo Bieber alikuwa bado hajapanda kwenye steji.
Shabiki
mmoja, Rikki Townsend, 16, alisema: “Kila mmoja alizomea. Wakati
alipofika hakusema hata ‘samahani’ – alianza tu kuimba.”
Baadae
Bieber aliomba msamaha mashabiki wake kupitia tweeter, akisema
uchelewaji wake ulisababishwa na sababu za kiufundi, na kuahidi kwenda
sawa katika shoo nyingine Alhamisi na Ijumaa uwanjani hapo.
Tukio
hilo limekuja baada ya staa huyo mtoto pamoja na kampani yake
kutimuliwa katika klabu ya Cirque du Soir jijini London Ijumaa iliyopita
kwa sababu wote walikuwa wakinuka harufu ya bangi.

Post a Comment