Dully awafunga midomo
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully
Sykes’, amekamilisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Funga domo
lako’ ambayo ameanza kuisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.
Dully kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Utamu’ ambacho
ameshirikiana vema na wakali wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na
Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Dully alisema
kazi hiyo tayari ameanza kuisambaza katika vituo mbalimbali vya redio
na sasa yupo katika harakati za kutengeneza video ya kazi hiyo.
“Kama ilivyo kawaida ya kazi zangu huwa haziwachoshi mashabiki wangu,
naomba wanipokee kwa mikono miwili na kazi hii ambayo naamini itawashika
mashabiki kutokana na ubora wa kazi hiyo,” alisema Dully.
Aliwaomba mashabiki wake wasichoke kumpokea katika ‘game’, kwani ni
mwendelezo wa kuwapa burudani zilizokwenda shule mashabiki wake.
Post a Comment