ad

ad

TAHADHARI KWA WANAOTAKA KUINGIA KWENYE NDOA

TAHADHARI KWA WANAOTAKA KUINGIA KWENYE NDOA
Jambo jingine ambalo kila mmoja anapaswa kulifahamu ni kwamba si kila mwanamume katika dunia hii ana sifa ya kuwa mume wala si kila mwanamke anafaa kuwa na mume.

Kuna wanaume wengi, kwa staili zao za maisha na hata afya zao duni, hawafai kuwa mume, pia wapo wanawake kwa staili zao za maisha na namna walivyo, hawapaswi kuolewa.

Hii ni mojawapo ya sababu kwanini kuna watu wengi hawajaolewa wala kuoa; pamoja na mambo mengine ni kwamba hawana sifa za kuwa mume wala mke. Maisha ni mazuri, lakini ni jambo muhimu sana kwako kutafakari kwa makini, kinyume na hilo ni vigumu sana kuwa na maisha yenye furaha.

Kama upo kwenye ndoa, na unaitaka furaha, angalia kwa makini matendo unayofanya, je yanachangia kuleta furaha au karaha? Wengi wanataka raha, lakini wenyewe hawana tone la raha, kitu ambacho si sawa hata kidogo. Ukitaka raha, toa raha. Je wewe huwa unatoa raha au shida tu nyumbani kwako? 
WATU wanakuwa na wapenzi si kwa sababu wanatafuta watu wa kuwatukana au kuwanyanyasa, bali wanatafuta raha.
       Mfanyie mazuri mwenzi wako ufurahie mwaka 2013
Mtu anapotafuta mpenzi, maana yake ni kwamba anatafuta mtu ambaye anaweza kukaa naye na kubadilishana naye mawazo katika kuendeleza maisha. Hakuna mtu ambaye anatafuta mpenzi kwa lengo la kupata mtu wa kumtukana matusi, kumtesa kwa namna yoyote. Hakuna mtu hata mmoja ambaye anatafuta mpenzi ambaye kesho na keshokutwa atakuwa anamkwaza.

Ukweli ni kuwa watu wanaingia kwenye uhusiano kwa lengo la kupata raha ndugu yangu. Je wewe ambaye unasoma makala haya mwenzi wako unamchukuliaje? Jibu unalo. Kuna wanaume wanawachukulia wake zao kama wafanyakazi wa ndani, wako tu wanaishi lakini hawapewi hadhi kama wake.

Kwa mfano unaweza kuona kuna miradi mbalimbali inaendelea, lakini hakuna cha maana ambacho mwanamke anaambulia. Kuna wanawake wapo tu, anachoambulia ni kupewa fedha ya kununulia nyanya. Wengine wamesoma lakini wamepigwa marufuku kufanya kazi na waume zao.

Mwanaume ambaye kweli anaipenda familia yake, bila shaka furaha yake itakuwa ni kuona mkewe anafanya kazi. Ndugu zangu maisha hayaeleweki, kuna watu ambao zamani walikuwa wana afya nzuri, lakini sasa ni vilema, wengine wamepooza miili na wengine wamefilisika.

Wengine ambao walikuwa mstari wa mbele kuzuia wake zao wasifanye kazi, sasa wanalishwa na wake zao.Wake zao ndio wanaoendesha nyumba kwa sababu labda anaumwa au pengine hana kazi ya maana anayoifanya.

Ninachotaka kusema katika makala haya ni kwamba kuna haja ya wapenzi kuangalia namna ya kufanyiana yaliyo mema; kila mtu ambaye yuko kwenye uhusiano, aangalie namna gani anaweza kumfanya mwenzi wake kuwa na amani.

Wengine wamesoma, lakini elimu yao na mafanikio yao yamekuwa ni sababu ya kuharibu nyumba zao; tuko kwenye sherehe kubwa hizi za mwaka mpya, wengine wanachowaza ni namna ya kwenda nje ya ndoa.

Ukimuuliza vipi anachosema hakina maana kwamba aaah unajua mke wangu hana mvuto, anavaa kizee na mambo mengine kama haya. Ni kweli inawezekana, lakini je wewe umewahi kutaka kumbadili awe kijana kwa maana ya kumnunulia mavazi mazuri na hataki kuvaa? Kama ulimpotoa kwao alikuvutia na sasa havutii tena, maana yake ni kwamba hauna malezi mazuri, hiyo ndio maana yake.

Ni vizuri kuangalia namna ya kufanya, ili kumfanya mwenzi wako aendelee kupendeza kama ambavyo ulimkuta awali, au zamani zile.

Kuna wanawake katika nyakati hizi za sikukuu wamekuwa hawana utulivu; dalili mojawapo ya mtu ambaye si mtulivu ni baadhi yao kuwa na zawadi ambazo hazijulikani zilikotoka au wengine kushindwa kuwa pamoja na mwenzi wake; wapo ambao wamekuwa wakianzisha safari kwa namna ambavyo wanataka wao.

Kwamba badala ya kuwa na mwenzi wake, anaweza kubuni safari kama vile kutembelea wazazi, kwenda kazini na mambo mengine kama haya.
Powered by Blogger.